Wakuu hapa tunachambua fesheni na mtoko kwenye nyumba za ibadaa " mfano tu ilipaswa kuwepo na BACKUP za mitandio/skafu au hata kitenge humo kanisani kutumika kama emergency cha kustiri uwazi/utupu huo" kama vile Hospitali kuna dawa za harakaharka za kuteremsha homa kali/tempretur kabla hujaanza kutibiwa" very simple kuweka standby.
Nakubaliana na Mr.Gefu kuwa kufukuza/kumkashifu ni kosa. Sasa hatorudi tena umeshampoteza zaidi ni bora kutumia hekima na busara kwenye UJAHILI kama huo, japo baadhi ya wanawake hukaidi na kuwa jeuri.!! Lakini jaribio ni bora!!
Hata angjitolea mwanamke mwenzie humAdvise kwa kuwa wasije vibinti vidogo kuanza kuiga na kudhani ni kawaida kutoka half-naked ktk nyumba za ibadaa!!
hapo sasa kwa upande wa kwetu kuanzia nyumbani hadi masjid watu wote hulindana na kutoa NASAHA (usia) ilikufuata heshima za dini na mavazi stahiki kwenye mkusanyiko au hadhara fulani, Laa sivyo matokeo na tija huwa halisemeki na hapatkuwepo utetezi au huruma.
" Jistiri kabla hujastiriwa (hujafedheheshwa) "