I wish: Ndio ninaweza, lazima nianze sasa!

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Nimefikiri, Nimewaza na kupata jibu moja: NDIO NINAWEZA, kwanini watu wengi wanafikiri watu wa Tanga hawawezi kufanya mabadiliko ya kisiasa, jibu rahisi UMWINYI,UDINI,WAVIVU n.k. (kama wasemavyo). Lakini je watu hawa hawawezi kubadilika? Kwanini, mimi ni mtu wa Tanga lakini ni mpinzani, nimebadilika? Kwanini mimi ni CHADEMA? Jibu rahisi: Kwasababu napenda kuona mabadiliko.Unaweza kuuliza mabadiliko gani, nina jibu kwa swali hili. Kwani mabadiliko haya hayawezi kuletwa na CUF.UDP,TLP,CHAUSTA n.k.? Jibu rahisi: Hawako tayari kufanya hivyo.

Ndiyo NINAWEZA, mwaka 2015 natumaini nitagombea ubunge jimbo la Lushoto kupitia CHADEMA. Imeshasemwa ni mapema mno kutangaza nia, lakini nina kitu ndani ya moyo wangu, this is my internal feeling, that i express to you na wananchi wote wakiwemo ndugu, rafiki, jamaa n.k ni ombi langu kuniunga mkono kwa hili.
 
Mgaya D.W

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
965
475

Mkuu mi nakuombea kila heri pamoja na kwamba ni mapema sana tafadhali hii yaweza kuwa njia njema wataz hasa wa Lushoto kuanza kukupima na kuona hazina ya maono yako kwaajili ya wanajimbo.Ninaamini unaweza na Mwenyezi Mungu akijalia waweza kuwa mwakilishi wa chama eneo kama mbunge 2015!
 
Komeo

JF-Expert Member
May 3, 2011
2,497
1,169
Nakutakia kila la heri, uwabadilishe na Wagosi wengine wa huko wanaofikiri kuwa mabadiliko ni dhambi.
Nakusihi usikatishwe tamaa na maneno ya watu wengine ukianzia humu humu JF kwa maneno ya kukatisha tamaa.
Pia usitishike na vitisho vya Shekifu (mbunge wa sasa), kwani mara nyingi maneno ya yule mzee hayafanani na umri wake, ni mzee wa kuropoka ropoka tu.
Best wishes.
 
Hiraay

Member
Jan 4, 2012
99
17
Nakutakia mafanikio, ingawa najua kuna kazi kubwa ya kuwabadilisha hao Wagosi. Matokeo ya kura za udiwani katika kata moja jimboni humo (Tamota) hivi majuzi hayatoi picha nzuri - CDM kura 312 vs CCM kura 901. Kwa hiyo ujue una kazi kubwa.
 
Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Nakutakia mafanikio, ingawa najua kuna kazi kubwa ya kuwabadilisha hao Wagosi. Matokeo ya kura za udiwani katika kata moja jimboni humo (Tamota) hivi majuzi hayatoi picha nzuri - CDM kura 312 vs CCM kura 901. Kwa hiyo ujue una kazi kubwa.

Heshima Mkuu, naomba nikuhakikishie hii ni indicator nzuri kwa CDM, kumbuka tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi CDM haijawahi kusimamisha mgombea kule, vilavile nguvu ya CDM bado haijaimarika vya kutosha, tegemea kuona mabadiliko zaidi, kazi inaendelea....
 
manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,067
10,707
Mbona Wagosi wapo na wanaweza au umesahau MAKAMBA'S and his Family?
 
kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,169
1,576
Kila la heri mkuu. Mwenyezi Mungu Awe nawe katika harakati zako za ukombozi wa nchi.
 
CRN

Member
Oct 24, 2012
60
8
Ndiyo unaweza,tena sana tu,nilistuka kidogo nilivyoona TANGA,nilidhani unataka kwenda kuchukua Diploma ya Sheria pale Lushoto ili baadae uteuliwe kuwa JAJI.
 
Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Ndiyo unaweza,tena sana tu,nilistuka kidogo nilivyoona TANGA,nilidhani unataka kwenda kuchukua Diploma ya Sheria pale Lushoto ili baadae uteuliwe kuwa JAJI.

BSc, Msc. Computer and Information Management...Copy that.
 
Hiraay

Member
Jan 4, 2012
99
17
Heshima Mkuu, naomba nikuhakikishie hii ni indicator nzuri kwa CDM, kumbuka tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi CDM haijawahi kusimamisha mgombea kule, vilavile nguvu ya CDM bado haijaimarika vya kutosha, tegemea kuona mabadiliko zaidi, kazi inaendelea....

Mkuu MG. All the best. Peeepooooooz....
 
High Vampire

JF-Expert Member
Nov 17, 2012
2,545
1,443
jipange kwelikweli na hela uwenazo za kuwapa wapigakura mim ntakuombea kwa mungu ili ushinde
 
Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
jipange kwelikweli na hela uwenazo za kuwapa wapigakura mim ntakuombea kwa mungu ili ushinde

Hili swala la kugawa pesa ni big challenge kwangu kutokana na uzoefu nilioupata kutokana na ushiriki wangu kwenye uchaguzi wa ubunge jimbo la Lushoto 2010 kama mpiga debe wa mgombea wa CDM na kazi kubwa ni kuondoa mind-set za namna hii, lazima tuanze kuelimisha wananchi majukumu ya mbunge, badala ya kumfikiria kama MFADHILI wamfikirie kama MTETEZI.
 
Mtoto wa tembo

Senior Member
Oct 4, 2012
198
30
Kwaiyo na wewe ni mdini,mwinyi na mvivu?

waziri wenu aliechaguliwa na jeykey ndio alitoa hayo matusi kwa wamama,wababa na wananchi wote wa Tanga,nashangaa mod katoa hiyo thread.unaonekana kama mgeni humu,hayo ni majibu ya waziri wako,sasa KANDA ndio kayapatia ufumbuzi.tatizo la viongozi wa sisiemu ni kutokujua wajibu wao.sanasana kam jibu analo ni kashfa na matusi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom