Kutumia neno I THINK katika hukumu linakuja kwa sababu mbili. Moja ni drafting techniques. Majaji wetu na mahakimu (baadhi) wamekuwa dhaifu sana katika kuandika hukumu. Unakuta hukumu haina mpangilio mzuri na hata fact hazieleweki. Wangine (kuna majaji sitataja majina yao hapa) wanaandikiwa hukumu na mbaya zaidi wanaowaandikia wanakopi format ya hukumu au ruling za majaji wengine, kinachofanyika ni kubadilisha majina ya parties na baadhi ya facts tu. Katika drafting techniques hizi unakuta jaji anatumia maneno ambayo hayafai katika uandishi wa hukumu ama ruling.
Mbili ni sababu ya kutojitambua kitaaluma. Jaji au hakimu anayo mandate, kwa hiyo anatakiwa atoe maamuzi yake kama mtu mwenye mamlaka. Neno I THINK halina mamlaka yeyote kisheria na hata kimantiki. kama mleta mada alivyosema, thinking yake lazima iwe guided na law, agreed judicial principles, and common sense.
Judicial thinking ni dhamira ya waandaaji hawa wa maamuzi. hata hivyo thinking hii, ambayo kimsingi ndio reasoning ya mahakama, haipaswi kuwekwa kwa mamna ya I THINK. Uandikaji wa hukumu nacho ni kipaji. hukumu zingine zinatoa maamuzi mazuri lakini hazina msaada wowote kwa wanaozisoma, hasa wanafunzi. Unakuta hata hazitoi msingi wowote wa kukumbukwa.