I phone | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

I phone

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by KyelaBoy, Apr 25, 2009.

 1. K

  KyelaBoy JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2009
  Joined: Nov 9, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zanguni siku hizi hapa Tanzania kuna wajasiriamali wanauza simu mtumba kutoka juu kwa bei poa hapa Dar,kwa kawaida hizo simu ikiwa mpya bei yake ni kubwa sana ,kwa watu kama sisi akina pangu pakavu hatuwezi kuzinunua ,lakini ni simu zenye vikorombwezo ambavyo ni muhimu sana kwa maisha ya siku hizi ,zina uwezo wa kuwa na vitu kama kamera,mziki na iternate.
  Sasa kuna pia sijui ni simu au ni nini sijui inajulikana kama I phones,hapo ndipo swali langu linaokuja je kwa mazingira ya Tanzania aina hii ya simu je inafaa kwa maana nimesoma tu kwenye mtandao kuwa ukitaka kuweka mziki sijui mpaka uende kwenye net ili uweze kupata I tunes.
  Kwa kifupi ningependa kujua kwa hapa bongo kama inaweza kutumika kwenye hii mitandao yetu ya simu hata ukiwa huko vijijini,na je batri yake ikiisha inakuwaje ?unaweza kununua wapi hapa bongo,
  asanteni
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,532
  Trophy Points: 280
  I-phone ni simu bomba sana tuu, ni mtandao wa kimarekani, ni dual band system inayotumika na software za macintosh, hivyo ili uitumie hapa bongo, lazima kwanza waiformat kwenye computer ya mac.
  Pia music wake ni i tune mpaka kwenye mac kama zilivyo i-pod.

  Hii simu ni kiboko, internet kama sms, touch screen tatizo ni moja tuu, haikubali 3G internet za simu za kibongo.
  Betri haina tatizo,nenda Mwembechai Plaza utazikuta za kumwaga. Ina ina memory mpaka 16GB!.
  Pia haina 'windows mobile'.
   
 3. K

  KyelaBoy JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2009
  Joined: Nov 9, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante sana Pasco,na je kuiformat nikiwa kwenye internate inawezekana au naweza kutumia njia gani kwa hapa bongo,pia nitaenda hapo Mwembechai kuangalia,thx alot
   
 4. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2009
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Iphone ni simu nzuri sana na vitu vingi sana kama vile Internet,Google earth,e-mail,kalenda,ipod,calculator,camera,notes na vingine vingi.
  Kuna iphone aina mbili moja ni ile iliyofungwa(Jailbreack)iphone aina hii huwezi kuitumia huku Bongo maana huwa imefungwa na inatumia mtandao wa AT&T ambao hauna coverage huku Bongo ila kama una iphone kama hiyo unaweza kuifungua na kuifanya iweze kutumia mitandao yoyote kama vile Vodacom,Zain,Tigo na kadhalika.
  Aina ya pili ni ile ambayo haijafungwa(unlock)iphone hii unaweza kutumia kwenye mitanda yoyote bila usumbufu wowote.
  Miziki yake inatumia Itune na inapatikana kwenye mitandao bure kabisa au kwa mtu yeyote mwenye computer na anayo hiyo program ya Itune.
  Hiyo itune itakuwezesha kuweka nyimbo kwenye iphone yako na kubadili mfumo kutoka mp3,wmv,wma na kuzifanya ziweze kuimba kwenye iphone yako.
  Iphone inaweza kuingiza na kuzicheza nyimbo zenye mfumo wa mp4 hivyo unaweza ku-convert nyimbo mbali-mbali kutoka mifumo tofauti-tofauti na kuziweka kwenye iphone yako najua utaifurahia sana.
   
 5. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2009
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Iphone pia inatumia internet haitumii WAP ya zian au vodacom bali inatumie EDGE kuiweka wala haina matatizo itafanyakazi vizuri sana kama una vodacom,zain,tigo,zantel au mtandao wowote ule.
  Iphone inatumia Rechargeable LITHIUM-ION battery ambazo huwezi kuzipata kariakoo wala duka lolote nchini.
  Battery ya Iphone yako ikielekea kuishiwa nguvu(inachukua kama miaka mitatu mpaka minne.)unashauriwa kuipeleka kwa service provider wa APPLE aliyekaribu nawe na utatozwa USD75.watakuwekea battery mpya kabisa.wewe hutakiwi kubadirisha battery ya iphone maana battery ya Iphone iko sealed huwezi kuiondoa wewe mtumiaji mpaka Dealer wa Apple.
  Tahadhali kuna Iphone ambazo si halisi zina kila kitu kama original lakini utazigundua kwa yafuatayo;
  1.Hazina nembo ya Apple
  2.Zina spare battery wakati Iphone halisi haina spare Battery.
  3.Bei yake ni ya chini sana bei iphone USD400-499.
  4.Ni nyepesi sana ukiishika wakati Iphone halisi ni nzito
  Earth-google utaweza kutembelea dunia yote na miji,vijiji vyote kwa wakati mfupi na kuangalia hata nyumbani kwako ukiwa wewe uko mbali sana.ina picha halisi,ramani ya miji,vijiji kutoka mita 200 juu angani.
   
Loading...