I- PHONE yasababisha kifo cha mrembo

I- PHONE yasababisha kifo cha mrembo

Verdy CB

Senior Member
Joined
Mar 19, 2013
Posts
149
Reaction score
67
Ma Ailun ... in flight attendant uniform
Inarepotiwa kwamba kampuni ya APPLE watengenezaji wa simu aina ya iPhone 5 wameanza uchunguzi baada ya maisha ya mwanadada mrembo pichani kukatishwa na kichao daiwa shoti ya umeme iliyo tokana na simu yake aina ya iPhone 5.

Ma Ailun, 23, alipatwa na shoti ya umeme wakati akijibu simu yake ikiwa kwenye charge inarepotiwa. Ajali hiyo mbaya hadi kufikia kupoteza maisha ya mrembo huyo ilitokea Alhamisi iliyopita nyumbani kwake Xinjiang Province nchini China.

Mrembo huyu ambaye alikuwa muhudumu wa kwenye shirika la ndege la China Sourthern Airlines na kuacha kazi hiyo hivi karibuni alinunua simu hiyo mwezi Desemba kweney duka la Apple nchini humo na alikuwa anatumia charger halisi ya Apple pia familia yake inareport.

Kaka yake amesema simu hiyo pamoja na charger yake vimekabidhiwa polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mzungumzaji wa kampuni ya Apple amesema: "Tunasikitishwa sana na tukio lilitokea na tuanatoa pole kwa familia ya Ma Ailun. Tutachunguza kwa kina na kushirikaina kikamilifu katika uchungunguzi wa jambo hili."

Tukio hilo limewapa wasiwasi watumiaji wa simu hiyo huku wataalam huko Hong Kong wakionya watu kuto tumia vifaa vyovyote vya umeme vikiwa kwenye charge (umeme).

Johnny Sin Kin-on, profesa katika chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia kilichopo Hong Kong amesema: "Kuna hatari ya kutumia kifaa cha umeme chenye betri wakati kikiwa kwenye charge (umeme), iwe shaver (kinyoleo) au simu."

Simu aina ya iPhone 5 imekuwa imekuwa ikipokea malamiko mengi toka iingie sokoni kutoka kwa wateja wake. Malalamiko yalikuwa pamoja na ubunifu (utengenezaji) wake kutokuwa mzuri, charger yake pamoja na apps yake ya rami kutokuwa na ufasaha.

Wiki iliyopita iPhone 5 ilionekana kuwa ni simu ambayo imepoteza umaarufu na mauzo yake kushuka sana nchini Uingereza. Na katika test za Benchmark pia imeonekana kuwa na NUSU ya speed, ukilinganisha na simu aina ya Samsung Galaxy S4 ambayo kwa sasa iko juu sana.

source: zeddylicious
 
Simu zetu zenyewe hizi dakika mbili tu jwi jwi jwi battery low sijui tutafanyaje.
 
Nimepata somo, kuanzia sasa marufuku kutumia simu iliyo kwenye umeme

Hii habari imeripotiwa sehemu nyingi. Mimi sio kama napingana nayo ila nimebaki na maswali luluki. Ninavyoelewa process ya kuchaji simu (iphone) ni kuwa kutoka kwenye soketi ya umeme kwenda kwenye chaja inaingia AC (alternating current ie 240 volts, 13 amps) na kutoka kwenye chaja kwenda simu inaingia DC (direct current ie 5 volts, 1.0 amps 5 watts). Sasa nimejiuliza: Alikufa kwasababu charger ilikuwa mbovu (haipunguzi umeme na ukawa unakwenda direct kwenye simu) au vingine? Kama jibu ni ndio, basi hata kama asingetumia simu, itakapojaa akaishika kutoa kwenye charger si angekufa tu? Nimepata mkanyiko naomba mwenye maelezo ya kitaalam atoe!
 
mchezo mchafu wa kuharibiana biashara, inaweza kuwa sababu. Tuwe na uhakika ni kweli imetokea?
 
Nimepata somo, kuanzia sasa marufuku kutumia simu iliyo kwenye umeme
mbona munaogopa kufa nyie.??. Ivi unajua kilichomuua mwenzio si lazma kikuuwe na wewe tu. Basi tu ni siku zikifika hata ukiwa unatembea utajikwaa kwenye jiwe na kufa hapo hapo
 
Hii habari imeripotiwa sehemu nyingi. Mimi sio kama napingana nayo ila nimebaki na maswali luluki. Ninavyoelewa process ya kuchaji simu (iphone) ni kuwa kutoka kwenye soketi ya umeme kwenda kwenye chaja inaingia AC (alternating current ie 240 volts, 13 amps) na kutoka kwenye chaja kwenda simu inaingia DC (direct current ie 5 volts, 1.0 amps 5 watts). Sasa nimejiuliza: Alikufa kwasababu charger ilikuwa mbovu (haipunguzi umeme na ukawa unakwenda direct kwenye simu) au vingine? Kama jibu ni ndio, basi hata kama asingetumia simu, itakapojaa akaishika kutoa kwenye charger si angekufa tu? Nimepata mkanyiko naomba mwenye maelezo ya kitaalam atoe!

kama umeme ulikuwa haupunguzwi cha kwanza simu ingeungua, nadhani kulikuwa na tatizo la continuity ya earthing kwenye Installation na hiki ndicho kilichomsababishia umauti.
 
Naongea kwa upande wa pili. Kuna vita kali sana ya kibishara kati ya samsung(china) na apple(u.s.a), so its kind of demarketing of competitor
 
Mimi nakubali kutokubaliana na huyo prof. wa Kichina eti tuepuke kutumia vifaa vikiwa vimechomekwa kwenye umeme na akatolea mfano shaver! Sasa utanyoaje bila kuweka kwenye umeme? INa maana anataka tuachane na mashine za HOME CUT?!!
 
Ana maanisha shaver zenye batery za kuchaji mkuu! tubadilike tu tuache ubishi mwanangu!
 
Ana maanisha shaver zenye batery za kuchaji mkuu! tubadilike tu tuache ubishi mwanangu!
Hapo nimekupata mkuu! Ila kwa simu hiyo ni noma sana, nilisikia kuna mwingine yeye alilipukiwa kimchina chake kilikuwa kwenye charger akaongea nacho muda mrefu wakamkuta hajitambui maana lilipuka kama bomu sikio lote kwao! Kupeleka hospitali jamaa wakapitiliza naye kwenda mortuary!!!

Kwa weli tubadilike mtazamo!!
 
Back
Top Bottom