I need a patriotic Injection | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

I need a patriotic Injection

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Speaker, Dec 9, 2011.

 1. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yes,..
  Wengi wenu leo hamjaenda kazini kwa sababu ni "Siku ya uhuru" wa Tanganyika na specifically
  mna sherehekea kufikisha miaka hamsini (50) ya uhuru huo.
  Binafsi sioni tofauti kati ya leo na jana au siku zote nilizoishi toka 14 march 1987.

  Yeah,najua wapo watakao sema kwamba nimezaliwa wakati wa mwinyi na kwa maana hiyo sijui
  "magumu" waliyo pitia wakati wa "kutafuta uhuru".....sidhani kama magumu ya wakati "wenu" ni
  makubwa kuliko magumu ni/tunayo pitia sasa.

  Sina "love" yoyote kwa siku ya uhuru,na so to say,...i don't feel anything like, love for Tanganyika.
  Au,kwa urahisi kabisa,sina uzalendo ndani yangu juu ya Tanganyika au Tanzania kama wengi wanavo iita.

  Sijilaumu kabisa,ila kama kuna mtu wa kulaumiwa juu ya mimi kutokuwa mzalendo basi ni "kila mtanganyika"
  ame sababisha hali yangu hii....Sikuwahi kujua raha toka nimezaliwa,toka naanza kusoma vidudu hadi leo hii
  napo malizia chuo kikuu...Kusoma ni kwa shida,maisha ni magumu kila jua linapo chomoza,maji hakuna,umeme hakuna
  Elimu ni ya kukalilishana vitabu na idea za wengine etc.

  Siijui kalamu inayo tengenezwa Tanganyika ikoje,penseli hatuna,wembe hatuna,njiti za kuchokonolea meno hatuna,
  pamba za kutolea uchafu sikioni hatuna,...lol

  Niliwahi kuwa mzalendo,nakumbuka nilipokuwa darasa la 4 hadi form1,nilipenda sana kuwa mpandisha bendera
  shuleni kila siku,nilikua kiongozi wa bendi (brass band) kuimba nyimbo mbali mbali zinazosifu Tanganyika na
  "LI CCM" kwa wakati huo...Nilikuwa scout nikilala porini mara nyingi kwa kudai eti "ni ukakamavu na kujifunza kuipenda
  Tanganyika"......all that is gone.Siipendi tena nchi yangu.

  Kama ilivyo kwamba uoga unaambukizwa ( Fear is infectious ),....tunakubaliana?
  Sawa,na unpatriotic is infectious,...na hapo ndipo napo kuja kwenye point yangu kwamba
  "Mmeniambukiza kuto kua mzalendo".
  Hakuna kiongozi wa serikali aliye mtanganyika kimatendo,
  Hakuna mwananchi anae ipenda Tanganyika kimatendo,
  Hakuna mwana JF anae ipenda Tanganyika kimatendo,..
  Hakuna mwana facebook anae ipenda Tanganyika kimatendo,...

  woooote hao ni watu walio nizunguka,na automatically SIIPENDI TANGANYIKA.
  Hayo yote yana udhihirisho mkubwa tu,viongozi wanaitafuna nchi kama vile wao wanatoka
  nchi jirani na sasa kuna mtu wana mkomoa,....
  sio viongozi wa serikali ya ccm wala wabunge wa upinzani,wooote ni wanafiki na wachumia matumbo.

  Watanganyika walidhihirisha kutokua wazalendo kama mimi pale walipoacha kuupigia mlima kilimanjaro uingie
  kwenye maajabu ya dunia,...sikuupigia pia na honesty kura yangu nilipiga kwa "Table Mountain",...

  Tanganyika sasa imegeuka kuwa "ng'ombe" alochinjwa na kila mtu ananoa kisu ili aondoke na nyama nono.
  Huo ndio uzalendo?
  Leo kuna wabunge wameandika facebook "happy birthday Tanganyika" na maneno kibao ya
  kupumbaza wapumbazika,....uhuni mtupu hakuna anae maanisha anachosema kwani hakuna asiyejua
  watu wanao rudisha nyuma maendeleo ya nchi hii ni wabunge,kwa kujilipa mishahara minono,posho nyingi na KUTOLIPA
  KODI.

  Sitakuja kulipa kodi,hadi walio niambukiza kuichukia nchi yangu wabadilike,....
  (usiulize ntakwepa vipi,maana napata mafundisho kwa kila anae nizunguka halipi kodi) ingawa najua
  inalipwa indirectly kwenye bidhaa kupanda bei.

  Leo hii,sherehe miaka 50 wananchi (wasio na kazi) wataenda uwanja wa uhuru,watachomwa jua,watapigwa njaa,..watatimuliwa vumbi na wataondoka na magonjwa lakini baadae,viongozi wataondoka kwenda kula kuku kwa mrija Ikulu.

  Wameshindwa nini kutoa chakula kwa kila mtanganyika leo nchi nzima?Don't tell me watakua wametumia hela nyingi
  maana tumezoea kutumia hata tusivyokuwa navyo,na hela nyingi zimetumika kwenye maadhimisho ya kila wizara.

  Watu vijijini wasingefurahia leo kupata "pilau" huku wakiambiwa ni siku ya uhuru atleast waikumbuke
  kwenye maisha yao?Kuna watu hata mlo mmoja hawapati lakini hata siku hii moja tu tumeshindwa
  kuifanya ya kujumuika kwa chakula kila mtanganyika.

  Badilikeni,Ipendeni nchi yenu na vizazi vijavyo vitaipenda pia.
  Otherwise,kila mtu ananoa kisu,...kikipata makali anakata nyama anayotaka na kukimbia.
   
 2. j

  janejean Member

  #2
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmh!! Inaonekana una hasira, punguza munkali kijana. we need u're plan!!!
   
 3. kulyunga

  kulyunga Senior Member

  #3
  Dec 9, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 146
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  Kakikua kataacha lol...
   
Loading...