I hate my wife

Hebu tujuze umri wako.
 
Kumchukia mtu ni dhambi kubwa hata vitabu vya Mungu vinatufundisha hivyo......samehe 7x70
 
msitukatishe tamaa na umalaya wenu! ulitegemea ukiwa na michepuko shetani akuangalie tu
 
Wanawake sijui tulikosea wapi jamani,,,,yaani unampenda mtu kwa moyo wote kumbe yeye anakuchukulia for granted namna hii? seriously?....Pole sana Mkuu kwa unayopitia, ila zungumza na mkeo wa uwazi na siyo kucheat.

Thanks sana. Unajua she was my only best friend. Yangekua mambo ya kuzungumzika na kuelewa basi yangekua yameisha. Katika maisha yangu sikujizoeza kua na marafiki wa karibu sana na mimi. Mimi muda mwingi nilikua nautumia home hasa kushinda na watoto wangu baada ya kazi. I like kids wangu sana so hua nawamis sana hata nikiwa kazini. Lakini kuna mambo ambayo nahisi ni muhimu mimi nijue kwanza yeye anayatangaza kwa watu kwanza mambo ya familia yangu sana. Mimi nikiyasikia hua nakaa kimya then unakuta analeta presha ili yale mambo aliyotangaza yatimie. Kuna siku alitamkia kwa macho naona kabisa bora angeolewa na X kuliko kuolewa na mimi. Nikikumbuka hili neno hata sina hamu nae kabisa. Moyo wangu umeshindwa kuhimili hili neno pamoja na mengine but hili ni kubwa kwangu. Nimepoa kifupi moyo umekua mgumu kumkubali tena kama nilivyomkubali mwanzo so nipo nipo tu.

Na kwa sababu sikua na marafiki wa karibu kiasi cha kushinda nao kwa stori za hapa na pale, unaweza kupata picha ni upweke gani nao pitia. Ni mazingira magumu sana kiasi hayaeleweki kabisa.
 
Nikupe pole tu Mkuu...

Ila usiendelee kujihusisha na hao wengine ambao huna mpango nao kuepuka kuwaumiza na kufanya mambo kua magumu zaidi.

Unahitaji muda wa kutulia na kujipanga upya kifikra

Ni kweli na hilo ndilo linanitesa moyoni mwangu sana. Kifupi nimeachana na karibia wote maana niliwaambia nimeoa but hawakusikia ni kama ndio nilikua nafungua mlango. NImebadili mawasiliano yangu hivyo wengi nimewaacha kabisa. Huyo mmoja ndio kichwa ngumu maana hata ukimpa viashiria kua kuna hatari wala hajali. Speed ni kubwa sana kiasi jinsi ya kuanza kumwambia ni shida kwa kweli ila kuna siku nitamuambia maana kusema kweli sina mpango nae kabisa. Ninajitahidi kupata ahueni ila hii relationship ndio inaniumiza kichwa nahisi wanangu watakosa raha sana lakini sina jinsi. Shida ni kua hata kuachana anavunga kama hataki wakati ukweli ni kua hatuwezani kabisa. Yeye anaona bora angeolewa na Z wakati mimi kwa mahali nilipo nahisi nahitaji kuishi peke yangu. Kama hali hii anaijua leo akiwa na watoto wangu ni ngumu kwa mimi kumuamini mtu mwingine tena.
 
Chaaaaa! Mm nikajua nitakutana na sehemu inayoelezea mapungufu kibwena ya mkeo yasiyoepukika wala kuvumilika kwa kuwa ww ni malaika hukoseagi kumbe kidemu kinakuzingua hadi unamchukia mkeo pasipo sababu.

Hata ukiowa huyo unayemuona mzuri ss baadae utajuta tn kwani mtazoena na pasipokuwa creative utarudi huku huku. Kwani awali ilikuwaje kwa huyu unayemchukia sasa.

Dogo, jichunguze kwanza wewe. Acha ubinafsi bana. Tengeneza chako. Alikutuma nani uwahi kuowa si ulimuona anakufaa km unavyomuona huyu. Jirudi dogooo
 
 
Duuh pole sana kaka kama una imani kweli funga siku 7 huku ukiwa unaamka usiku wa manane unasali kwa imani mlilie Mungu shida zako zote nakuapia kila kitu chako kitakaa sawa na akili yako itatulia.

Asante kwa ushauri mkuu. Maana maisha yangu yamebadilika ghafla sana na sioni ndoto nilizokua nazo tena.
 
 
Kwa mara nyingine pole mkuu... Huyo kichwa ngumu usichoke kumueleza ukweli wa moyo wako kwamba huna future nae...

Akiendelea kushupaza shingo hiyo itakua ni shida yake sasa. Pia kwasasa tafuta kampan utakayoona inafaa kwako,pendelea kujichanganya kadri uwezavyo kwa watu utakaoona wataleta ahueni kwako.

Ukiendelea kua mpweke na kutojichanganya itakua ngumu kupata unafuu,fanya vitu vitakavyo kufanya urilax ili kuruhusu mawazo mapya na chanya kuzaliwa....

BTW usikumbatie sana mawazo ya upweke jua kwamba changamoto na makwazo ktk maisha haya tuliyonayo hayana budi kukupata.

Katika hali hiyo kua mtu wa ibada mtegemee Mungu nae atakuvusha salama na kukupa amani yamoyo. Kama ni msomaji wa biblia anasema "njoni kwangu ninyi nyote mnaolemewa na mizigo mizito nami nitawapumzisha,jitieni nira yangu mjifunze kwangu kwakua mimi ni mpole na mnyenyekevu wamoyo"

Mstari huo na mingine ni moja ya mistari unayoweza kutumia ikakuvusha katika ugumu ulionao mpendwa.
 
Ndoa si jela, ndoa Ni hiari yako na unatakiwa kuifurahia, kumbuka Kuna maisha baada ya devorce. Mpunguza kulalama na uwe mtu wa vitendo. Ww si wa kwanza
 

daahh!bora ex!!pole sana

au uko busy sana na kazi?

na yy ni mfanyakazi pia?
 
unajua wanaume mnavituko sana!
yaani unakua na mahusiano huko halafu unakua unamcompare wife na kimada...
unalazimisha wife awe the best kama kimada!
ukiuziwa na kimada unahamishia hasira zote kwa wife!
Halafu kwa nini uone mabaya ya mtu tu?
huyo mkeo hana jema kwako? kwa nini usihesabu japo mema yake machache?
anyways wewe si mkamilifu kumtaka mwenzio akamilike.
Safari njema kwenye maamuzi yako.
 

Kwa kusoma haraka haraka naona bado una hasira sana ma mkeo na pia huja-identify mizizi ya tatizo/matatizo ya ndoa yako..... Chanzo cha matatizo ni nini hasa.... nafikiri ungeanza kutafakari kuanzia hapo.... otherwise unachokiona ni output/product/matunda ya chanzo cha matatizo yaliyopo kwenye ndoa yenu.... Pole sana.
 
Mkuu sijui kama umeshasaidiwa tatizo lako au LA (ndo nimeona hii kitu leo). Ushauri wangu ni huu: the later the worse. Usijaribu kuwa mkakamavu kwenye tatizo serious kama hili. Share kiss kizima tukupe mawazo uondokane na tatizo. Usiendelee kusubiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…