Habari wakuu!naomba msaada wa kitaalamu kuhusu gesi ya hydrogen,inafaa kwa matumizi ya kupikia,nimegundua njia rahisi ya upatikanaji wake,naomba kwa enaejua anijuze,naomba asitumie maneno ya kitaalamu sana kwani mimi elimu yangu ni ya kawaida sana,maelezo yawe ya kiswahili na mepesi kueleweka,natanguliza shukrani zangu kwenu
Ndugu hiyo gas ni hatari wala usijaribuHabari wakuu!
Naomba msaada wa kitaalamu kuhusu gesi ya hydrogen,inafaa kwa matumizi ya kupikia, nimegundua njia rahisi ya upatikanaji wake,naomba kwa enaejua anijuze.
Naomba asitumie maneno ya kitaalamu sana kwani mimi elimu yangu ni ya kawaida sana, maelezo yawe ya kiswahili na mepesi kueleweka.
Natanguliza shukrani zangu kwenu.
Ndugu hiyo gas ni hatari wala usijaribu
kuangaika nayo inaweza kukuletea madhari,
labda kama una kiwanda cha kutengeneza milipuko
inaweza kukufaa.
nashukuru mkuu,kwa maelezo yako kwamba gesi hiyo inaweza kuendesha mitambo na kukatia vitu,ila hujanieleza kama inafaa kwa mtumizi ya kupikia!kuhusu kutoa elimu hii tufanye subira,kwani inaweza kuharibu biashara za watu,ila naomba kupata elimu zaidi kuhusiana na gesi hii
Haifai kwa kupikia mkuu...jibu hilo lakutosha??...ni gesi hatari ina ptoperty za kulipuka
Naomba jibu la swali hili, kama umesema wewe sio expert, je umejuaje kua hiyo ni hydrogen?
Kama unajua ni hydrogen basi lazima utakua unajua na properties zake pia, umekuja hapa kutupima akili.
Haya tukirudi kwenye mada, natoa jibu kusaidia wengine wanaotaka kujifunza ila sio wewe coz unatupima akili.
Hydrogen ina-burn na inaweza kutumika kwenye kupika, lakini kuna sababu za msingi za kwa nini usiitumie kwenye upishi.
Kwanza ni usalama wake, hydrogen haina harufu kwa hiyo in case ime-leak chumba kizima hutojua, utawasha flame nyumba italipuka.
Pili, ukiwa unapika kwa kutumia gas mara zote unahitaji kuona flame ili ufanye regulation ya amount of heat unayotaka, hydrogen ikiwa inaungua inatoa white flame, so hutoweza kuona vizuri we utashangaa tu heat inaongezeka, hutojua kama umeweka moto mwingi au la, unaweza zidisha kumbe flame imejaa sufuria zima kwa hiyo its a waste.
Hizo sababu zinatosha kabisa kukufanya usijaribu kuichezea kabisa.
Nilizani wana JF hawataki kukutendea haki uzi wako wala kukupa idea ya wanayo fahamu kuhusu hiyo gas....Kumbe wewe mwenyewe una ubinafsi unaulizwa umewezaje kujua kama hiyo ni H hutaki kutoa somo....Sijui unahisi ukitoa somo tuta tajirika sio???
Watu kama nyie ni wakuupuzwa maana hamna msaada kwenye jamii...Unataka kuexplore idea za watu lakini wewe hutaki kutoa idea zako....Shame on You