Hydroelectric power

Hydroelectric power

ramstag

Member
Joined
May 12, 2015
Posts
22
Reaction score
2
Wadau habar.
Naomba kuuliza hiv katika project za hydroelectric power haiwezekani maji kuyarecycle ili yaendelee kutumika na kulinda vyanzo vingine vya matumiz ya maji?
 
kuyarecycle
una maana urudishe maji mlimani ?
maana kuzalisha umeme maji inabidi yashuke kwenye kilima ( mfano wa dam )

kwa Tz, Rufiji Basins itakua mradi wa kwanza kuweka 'Pumped Storage Plant' , ni ghali mno
Turbines (PAT) zilezile zitatumika kurudisha maji juu ( reservoir ya juu ) na sio mda wote
ni kwa masaa machache ndani ya masaa 24
 
Ndicho nilichomaanisha
Nimewaza hili kutokana na mgogoro wa mto nile.Kwa mantiki hiyo hata nile wanaweza hiyo kitu wakapunguza mgogoro.asante kwa ufafanuzi
 
Ndicho nilichomaanisha
Nimewaza hili kutokana na mgogoro wa mto nile.Kwa mantiki hiyo hata nile wanaweza hiyo kitu wakapunguza mgogoro.asante kwa ufafanuzi
Hiyo ni sawa na kutembea hatua tatu mbele halafu ukarudi nyuma tano. Kupata nishati ya maji kutoka mlimani haina gharama kwa kuwa jiografia teyari iko hivyo, maji yanateremka tuu. Ila kuyarudisha bwawani ambapo ni juu utatumia gharama kubwa, kwa hiyo haina maslahi.
 
Wadau habar.
Naomba kuuliza hiv katika project za hydroelectric power haiwezekani maji kuyarecycle ili yaendelee kutumika na kulinda vyanzo vingine vya matumiz ya maji?
Mkuu INAWEZEKANA kwa kutumia njia inaitwa Hydro Pumped storage na hio ndio habari na mpango mkubwa wa nishati duniani kwa sasa ambapo nishati inazidi kua adimu.

TULIA VIZURI
Ipo hivi Matumizi ya umeme yanatofautiana kwa Majira(usiku na mchana)
Mfano maeneo yenye viwanda Mchana kunakua na demand kubwa sana ya umeme sababu ya kuendesha mitambo inayohitaji umeme mkubwa.

Maeneo yenye makazi ya watu usiku mahitaji ya umeme yanakua makubwa sababu watu wanarudi majumbani na ku washa vifaa vingi vinavyotumia umeme mfn Taa, Tv, fridges, pasi, heater, majiko ya umeme n.k

Generally kwa takwimu zinaonesha mahitaji ya umeme usiku mpaka asubuhi yanakua makubwa zaidi ya mchana.

Sasa hapa twende kwanza kwenye vyanzo vingine vya nishati nikiwa specifically (Upepo na Jua) hapa sasa ndio jibu lako linapatikana

Wakati wa mchana kuna kua na jua kali na pengine na upepo mkali, hapa tutazalisha umeme wa aina mbili, Solar and wind energy,
Kumbuka mda huu matumizi ya umeme ni madogo...
sasa angalia hapa, mchana kunakua na matumizi madogo while uzalishaji mkubwa.
Unaweza ukajiuliza kwa nini mda huu sasa umeme usiwe cheap sababu ya vyanzo vya uzalishaji ni vingi na mahitaji ni madogo?
Simple answer ni kwamba huwezi uka control nature, namaanisha huwezi ukapunguza kasi ya upepo au nguvu ya jua, hivyo gharama za uendeshaji zinabaki zile zile, kinachotokea sasa,

Gridi ya umeme wa maji wananunua ule umeme wa ziada kutoka kwa umeme wa Upepo na Jua mfano kwa Tsh 1000,
Huu umeme utatumika sasa kupandishia maji kutoka chini kwenda Juu(Lower to upper reservoir), lazima wauze sababu wanazalisha umeme mkubwa na mahitaji yanakua madogo na cost ya ku control ni kubwa zaidi ya kuuza..

Ikifika usiku tayari bwawa litakua limejaa maji, basi wanayaruhusu yashuke tena,
Hapa sasa watauza umeme wao kwa Tsh 2000, bado watakua na faida ya tsh 1000.

Kuna maelezo mengi nimeshindwa kuyaweka ili kutochosha watu, unaweza uliza swali lolote nitajibu iwapo nina ufahamu nalo.
 
una maana urudishe maji mlimani ?
maana kuzalisha umeme maji inabidi yashuke kwenye kilima ( mfano wa dam )

kwa Tz, Rufiji Basins itakua mradi wa kwanza kuweka 'Pumped Storage Plant' , ni ghali mno
Turbines (PAT) zilezile zitatumika kurudisha maji juu ( reservoir ya juu ) na sio mda wote
ni kwa masaa machache ndani ya masaa 24
Mku upo sahihi, ila naona gharama kubwa ipo kwenye kuweka mfumo wa Pumped storage plant(specifically Francis Hydraulic pump) ila uzalishaji sio sana
 
Ndicho nilichomaanisha
Nimewaza hili kutokana na mgogoro wa mto nile.Kwa mantiki hiyo hata nile wanaweza hiyo kitu wakapunguza mgogoro.asante kwa ufafanuzi
Mi naona niles wanaweza tena kwa kiasi kikubwa sana zaidi ya wengine,
Hasa ukiangalia wao wapo ukanda wa jangwa amabao una jua na upepo mkubwa na hivi ndio backbone ya recycling ya umeme wa maji.
 
Back
Top Bottom