Huzuni: Boss kajilipa cash kuhamia Dodoma,Mimi mwaka wa pili hajanilipa uhamisho

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
4,020
3,657
Jana nimekutana na Mtumishi mmoja mitaa ya Ilala akanipa huzuni. Huyu jamaa ni mtumishi wa serikali. Kaniambia, Boss wake alimhamisha kituo cha kazi miaka miwili imepita. Hakumlipa fedha ya uhamisho. Amefuatilia mara nyingi,kaambiwa hakuna hela.

Bossi wake huyo, kapata uhamisho mwezi jana kwa utaratibu wa Idara za Serikali kuhamia Dodoma. Alivyonieleza, boss wake huyo amejilipa cash stahiki zake zote za uhamisho! wiki moja kabla ya kuhama. Nimejiuliza, kumbe huko utumishi wa umma kuna madaraja ya aina hiyo?

Kuwa wale watumishi wa chini hawana umuhimu sana kiasi wacheleweshewe haki zao kiasi hicho? Huyu jamaa nimemhurumia sana na kanihuzunisha.
 
kosa alilolifanya ni kuhamia kituo kipya kabla ya kulipwa stahiki zake. Kanuni inamruhusu kugoma kuhama kabla ya kulipwa. Kama alihama kwa gharama zake kumbe pesa anayo so atulie atalipwa arrears yake
 
let this post not distract my focus in carrying boxes here!
 
Jana nimekutana na Mtumishi mmoja mitaa ya Ilala akanipa huzuni. Huyu jamaa ni mtumishi wa serikali. Kaniambia,Boss wake alimhamisha kituo cha kazi miaka miwili imepita. Hakumlipa fedha ya uhamisho. Amefuatilia mara nyingi,kaambiwa hakuna hela. Bossi wake huyo, kapata uhamisho mwezi jana kwa utaratibu wa Idara za Serikali kuhamia Dodoma. Alivyonieleza,boss wake huyo amejilipa cash stahiki zake zote za uhamisho! wiki moja kabla ya kuhama. Nimejiuliza,kumbe huko utumishi wa umma kuna madaraja ya aina hiyo? Kuwa wale watumishi wa chini hawana umuhimu sana kiasi wacheleweshewe haki zao kiasi hicho? Huyu jamaa nimemhurumia sana na kanihuzunisha.
Yaani serikalini ni majanga, with some few exception kwa vyuo, ila sehemu zingine zote iwe agency, ni majanga. Halmashauri ndiyo dudu kama lishetani, wafanyakazi hawapendani, ni visa na mikasa, chuki na kuoneana wivu, kuuana na kulogana ndiyo jadi yao. Na ndiyo maana kuna umuhimu wa kuwaelimisha wafanyakazi wa serikali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom