Balozi ni utambulisho wa watu wa taifa fulani katika nchi ya kigeni..., ni mwakilishi na msemaji wa mkuu wa taifa fulani ktk nchi ya kigeni... Kwa maana hiyo aidha watanzania ndio machekibob au rais wetu ndo chekbob.. maana quality unazoziona kwa balozi ni reflection ya quality ya wale anaowawakilisha.Kwa anayejua naomba kufahamisha hawa mabalozi wa heshima huwa wanapatikana vipi, maana huyu bwana Robert Shumake ambaye tunaambiwa ni balozi wetu wa heshima US, naona pia ni balozi wa Botswana at the same time (Mr. Robert Shumake Bio | Honorary Consul of the Republic of Botswana), Hii ni halali au?..halafu vigezo huwa ni vipi mbona jamaa kama chekbob fulani hivi na mie nishazoea balozi huwa mtu mzima...Anyway naomba tujadili.
Robert Shumake ni jasusi wa CIA,nyie kumbe hamuwajui wamarekani,majasusi dizani ya shumake wametapaka dunia nzima,na huwezi kuwagundua,wengine wako ubalozini wakitambulishwa kama afisa balozi,wengine wapo ktk mashirika ya misaada,wengine huja kama wakufunzi wa kijeshi,'military trainer'na wengine huja kama mapadri,CIA si ya mchezo,ndo taasisi ya serikali ya US iliyoajiri watu wengi kuliko taasisi yoyote ile.