Huyu ndiye yuleyule Magufuli, au tumtarajie mwingine?

A Lady

Senior Member
Apr 28, 2009
103
0
Simtetei Magufuli ! Ila ni kati ya wale watendaje ambao wanauma na kupuliza. Kuna wengine wanauma hata mfupa hawaachi.
Ila inshort ni MAAFA tu.
 

nickname

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
524
225
Mimi naishia hapa,Magufuli si fisadi na nitaendelea kuamini hivyo mpaka kufa
 

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,194
2,000
Crashwise maswali yako ni mazuri naomba mtumie mbunge wako akamuulize waziri bungeni utapata majibu safi toka Wizarani na sio hapa
Kama hunajibu siyo lazima uandike, Inamaana mleta mada hana mbunge kwanini huja mwambia ampelekee mbunge wake

Crashwise,

..hoja ya serikali ilikuwa kwamba nyumba za serikali ni za zamani mno, na serikali inaingia gharama kubwa kwa ukarabati.

..sasa hapo ndipo wajanja kina Magufuli wakaja na idea kwamba nyumba zile ziuzwe na fedha zitakazopatikana zitumike kujenga nyumba mpya.

..Magufuli akawahakikishia wabunge waliokuwa na mashaka kwamba uuzaji wa nyumba zile utawezesha ujenzi wa nyumba mpya 100%.

..tatizo lililojitokeza ni kwamba Magufuli na wakubwa wenzake serikalini wakaamua kuuziana kwa bei poa, which was way below what those houses and plots would have brought in an open market.

..baada ya serikali kushindwa ku-raise enough funds za ujenzi wa nyumba mpya, Magufuli akarudi tena bungeni na kuomba fedha. yaani sasa wananchi tukalazimika kulipia hasara waliyotuingiza viongozi vibaka.

..MAGUFULI AWE MFANO KWA KUTUBU MAKOSA YAKE, KUTUOMBA RADHI WANANCHI, NA KURUDISHA SERIKALINI NYUMBA ALIYOJITWALIA.
Mkuu JokaKuu

asante sana kwa majibu yako
 

mark sam

Member
Oct 16, 2014
49
95
..kama Magufuli alikuwa hakubaliana na uamuzi wa KUIBA nyumba za serikali basi angejiuzulu. mbona Mtei hakukubaliana na bosi wake na akachukua uamuzi wa kujiuzulu?

..si kweli kwamba angejiuzulu basi angefulia. huku mitaani Magufuli alikuwa akijulikana kama muadilifu, kwa hiyo kama angekataa kushiriki WIZI ule basi jamii ingemkubali zaidi kama mpambanaji wa kweli.

..kama Magufuli alikuwa anaogopa kujiuzulu basi walau yeye binafsi angeepuka KUIBA nyumba zile. kitendo cha Magufuli kujitwalia nyumba ya serikali kinathibitisha kwamba alikuwa anakubaliana na uamuzi ule 100%. zaidi kuna tuhuma kwamba Magufuli alikwenda mbali zaidi na kuwashirikisha hata ndugu na vimada ktk wizi ule.


..Magufuli pia anahusika kuiingiza serikali hasara ya shilingi bilioni 14 kutokana na kiburi chake cha kukaidi ushauri wa kitaalamu na kuamua kuvunja kituo cha mafuta kule Mwanza. mmiliki wa kituo cha mafuta alikwenda mahakamani na kushinda kesi.

..zaidi, kuna taarifa za Magufuli kupendelea jimbo lake ktk mradi wa ujenzi wa barabara.

NB:

..kinachomshinda Magufuli kutubu makosa yake na kurudisha nyumba aliyoiba ni nini?
Magufuli hoyeeeeee!!
 

bendaki

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
954
250
1. plot zile sasa zina thamani ya mabillion. 2. Nyumba zile zilikuwa karibu na maofisi mufanyakazi angeweza kutembea kwa mguu. 3. Sasa wanaishi mahotelini au wamepata nyumba nje ya miji kila Siku kwa sababu ya traffic jams wanafika ofisini saa 4.00 na kuanza kutoka mapema. nk nk.
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,179
2,000
Hoja ni kuwa hatufai kwa mengi tu! Na kuna wizi wa kutisha tanroad ambao ulisemewa na boss mpya wa CAG na hakuna majibu hadi sasa. Kivuko cha bagamoyo ni mfano mwingine na hakuna meneja wa tanroad hata mmoja aliyefukuzwa kazi kwa ubadhirifu.
Na hii mishangao yake (mashikolo) ya huduma za jamii uwa mbovu ni kutuhadaa tu hakuna jipya atakaloweza kufanya kwani sumu ni ileile kinachobadilishwa ni bomba la sindano tu. Tumkatae kwani lengo lake ni kwenda kuwalinda mafisadi wenzake waliojaa uoga wa kwenda segerea.
 

Yodoki II

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
4,881
2,000
Hzo nyumba zilikuwa za Watanzania,wamepewa Watanzania shido ipo wapi?Zaıdı hapa nı wivu.Hatuwezi nufaika sawa hata tungekuwa wajamaa kwa kiwango cha juu kabisa!!
 

libra

JF-Expert Member
May 23, 2013
302
225
Hivi ile kesi iliyopewa jina mtaani "samaki Wa magufuli"iliishaje?serikali ilishinda kesi!,maana magufuli aliishupalia sana!
 

mkezwag

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
3,245
1,500

Magufuli hakuuza nyumba za serikali,kuuza nyumba za serikali ulikuwa uamuzi wa baraza la mawaziri chini ya Mwenyekiti ambaye ni Rais.
Wizara aliyokuwa akiiongoza Magufuli ndiyo iliyopewa jukumu na baraza la mawaziri kuuza hizo nyumba.Katika serikali mawaziri hufanya kazi kama timu,uwajibikaji wa pamoja.Baraza la Mawaziri likishaamua wewe uliyepewa agizo ni utekelezaji tu.


Mwakyembe alikuwa Mwenyekiti wa kamati teule ya bunge na alichaguliwa na Bunge,kufanya kazi kama alikosea basi Bunge lingemwajibisha.Yaani wabunge wote 289 hawakuona kosa la Mwakyembe ukaona wewe ,kwa hiyo walikuwa wajinga kumuacha aendelee kuwa Mwenyekiti au wewe mtu mmoja ndiye.??

Kwa Magufuli na Mwakyembe huna hoja .----!!
Ccm bana mnanifurahisha sana,kwenye uuzaji wa nyumba za umma mnasema ni baraza la mawaziri liliamua ila kwenye issue ya Richmond baraza la mawaziri na mwenyekiti wake hawatajwi,janga kweli kweli
 

mkezwag

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
3,245
1,500
Hzo nyumba zilikuwa za Watanzania,wamepewa Watanzania shido ipo wapi?Zaıdı hapa nı wivu.Hatuwezi nufaika sawa hata tungekuwa wajamaa kwa kiwango cha juu kabisa!!
Mkuu umetisha sana,yaani hata Escrow si ufisadi na wazungu kutunyima misaada wanatuonea wivu maana ile pesa ilikuwa ya watanzania na waligawana watanzania.

magufuli aache kudanganya umma Kwamba ataanzisha mahakama ya kumhukumu mafisadi maana mafisadi ni watanzania na wana fisadi Mali ya watanzania aache wivu wake wa kike,atavalishwa kanga kwenye jukwaa?
 
Top Bottom