Huyu ndiye baba yetu

Aliishi aliyoyaamini hata kama alikuwa amekosea....tofautisha maeno na matendo ya viongozi wetu wa sasa!
 
Hongera sana Mwalimu Nyerere, ulionyesha kwa vitendo kuikomboa nchi hii.
Lakini hawa wakombozi wapya wanajiita Chadema wanatumia helkopta kwa mambo ya kijingajinga tu.
POSHO na malupulupu mbele.
"Siwezi kukosa Nyama ya kuchoma" Dr.Slaa
 
Anastahili kabisa kuitwa baba wa taifa letu
kwa sababu Mtwara walitembea uchi, kombe la dunia tulikuwa hatulioni enzi zake, wala ligi kuu ya ulaya na spain. tena hata Neymar tusingemjua! halafu hati miliki ya wanamuziki kuwasaidia kuinua maishao, Yanga na simba kujiendesha kibiashara, Kuwepo kwa Azam nako haya yote yasingetokea! kwangu mimi huyo mzee alikuwa ni baba wa kambo!
 
Tofautisha nyakati mkuu
 
Ukiwa una mbeza pima akili yako ujinga wake na mapungufu yake ww ndo mafanikio yako!!!
 
nyie mnasema tu. unajua icho kiatu kilikua kinauza bei gani kipindi hicho? inaweza kua ndio viatu bei mbaya zaidi kwa wakati huo. baada ya miaka 30 kizazi chetu wakionyeshwa picha ya kikwete ya sasa watasema "huyu raisi alikua hana gari zuri" kumbe hilo gari itakua limepitwa na wakati....ndo kama sisi na nyerere
 
tusingekuwa na TV station, internent na simu za mikononi! mtwara s,ruvuma na Lindi tungetembea uchi sana!

mtazamo wako tu,dunia inabadilika sana tu,mabadiliko huwa hayazuiliki.sasa leo hii tuna nini kwani kila shilingi ya nchi hii na rrasilimali za nchi hii zinaishia mifukoni mwa watu ambao si zaidi ya 50 wakati nchi nzima ina watu 45milioni.sasa faida iko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…