Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,291
- 2,468
Yule wa WCB. Kiukweli naye huyu sikjua katokea wapi, mara nikamwona kasajiliwa na Wasafi. Nikimsikiliza nasikia kile ninachopenda kusikia, yaani sauti nzuri ya uanamuziki. Nikajisemea kuwa Diamond hakukosea.
Sasa kuna hii music video ya Madee inaitwa Paulina. Sio maarufu sana kwenye redio au tv bali you tube. Nilikutana tu na huu wimbo nikaupenda na nikawa nautazama mara nyingi. Aliyenivutia sana ni huyo kijana aliyeshirikishwa na Madee. Kaimba vizuri sana. Nikawa najiuliza sasa huyu katokea wapi? Na baada ya hapo mbona sijawahi kumsikia au kumwona tena? Nikajisemea hakika vipaji vinapotea. Maisha yakaenda. Nikawa nausikiliza hasa wakati huyu dogo anaimba. Nikawa nasikitika kipaji kimepotea.
Sasa leo tena napitia nyimbo hizi nakutana na huu wimbo. Ilipofika zamu yake nikamtazama sura vizuri nikajisemea huyu si Raymond? Nikajiaminisha hivyo. Hakika niliposoma jina lake kwenye Madee ft Raymond nikajisikia faraja kuwa kipaji hakikupotea. Kumbe ni Rayvanny huyu wa WCB. Hakika kipaji hakimtupi mtu. Huyu Raymond wa Paulina sio wa Natafuta kiki. Big up Ray. Big up Diamond.