Huyu nabii George Kairuki ni nani?

Huyu nabii George Kairuki ni nani?

Socw

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Posts
1,385
Reaction score
2,850
Muda huu anaendelea kuhubiri hapa mtaani kwetu kuhusu Kanumba na Diamond kuwa ni ma 'freemason, tena anasema ana mafuta matakatifu kutoka kwa mungu ambayo atayatumia kuangamiza dunia anasema aliyaonyesha dah! Mji mzima ulipatwa na taharuki na kusema yeye ni nabii.

Ni kijana tu, amenyoa kiduku, t shirt lina mistari, ana suruali modo nyeupe amekuja na kagari kadogo ka 'kirikou' samahanini kwa kuandika bila mpangilio maana nipo kwenye msongamano wa watu.

Naomba mwenye taarifa za huyu mtu anipe

Chanzo: Mimi mhudhuriaji

Eneo: Dodoma, Bahi mission, eneo la Singidani
 
muda huu anaendelea kuhubiri hapa mtaani kwetu..kuhusu kanumba na diamond kuwa ni ma'freemason..tena anasema ana mafuta matakatifu kutoka kwa mungu ambayo atayatumia kuangamiza dunia..anasema aliyaonyesha dah mji mzima ulipatwa na taharuki na kusema yeye ni nabii..ni kijana tu, amenyoa kiduku, t shirt lina mistari,ana suruali modo nyeupe..amekuja na kagari kadogo ka 'kirikou' samahanini kwa kuandika bila mpangilio maana nipo kwenye msongamano wa watu..naomba mwenye taarifa za huyu mtu anipe

source: mimi mhudhuriaji
eneo:dodoma, bahi mission, eneo la singidani
Huyo jamaa nimeshawahi kumsikia hadi redioni. Nilimsikia kwa mara ya kwanza kipindi kile Kanumba amefariki. Anaeleza ushuhuda kwamba yeye pia alikua freemason ila alifanikiwa kuacha uanachama bila kudhurika. Anasema ameokoka yupo imara.. Freemason wanataka wamuue wanashindwa. Kama ni George huyo basi hizo ndio dondoo zake kwa ufupi.... Lakini nikuulize, Bahi kuna eneo linaitwa Singidani?
 
Magufuli kweli kiboko kabana watu wamesha anza kuchanganikiwa!
 
HUYO JAMAA ALIKUJA HATA HAPA KONGWA....
 
Hivi bado tu kuna watu wanatapeliwa na huyu jamaa???
Alishawahi kufake kifo chake mwaka 2012 nadhani ili baadae aje kujifanya amefufuka lakini watu wakamshtukia na akaomba radhi mpaka kwenye magazeti.. Daah inasikitisha kuona bado kuna watu anawalia hela zao!! Lakini ndio maisha, wajinga ndio waliwao
 
Nadhani hapa ungeelezea kwa undani tungefaidi zaidi
 
Nabii kanyoa kiduku,suruali modo,...Safi nabii endelea kula hela za wajinga..
 
Matapeli ni wengi sema wanatofautiana kwa maneno na style zao
 
Hivi bado tu kuna watu wanatapeliwa na huyu jamaa???
Alishawahi kufake kifo chake mwaka 2012 nadhani ili baadae aje kujifanya amefufuka lakini watu wakamshtukia na akaomba radhi mpaka kwenye magazeti.. Daah inasikitisha kuona bado kuna watu anawalia hela zao!! Lakini ndio maisha, wajinga ndio waliwao
Nalikumbuka sana hili tukio. Alijifanya amekufa akawekwa kwenye sanduku na kuagwa akajidai anapelekwa Kenya kuzikwa. Waandishi wa habari wakaalikwa kuja chanika kushuhudia tukio hilo.

Gazeti la udaku la Kiu ndio walishtukia mchezo. Wakamchomoa alikokuwa amejificha ili Siku ya Tatu ajidai kafufuka kama Yesu. Alipohadithiwa mchezo mzima akaomba msamaha
 
WA matendo haya...huyu ni tapeli tuu.
 
huyu si yule jamaa mwenye macho mregezo kama shoga.. aliwahi kujidai amekufa afu wajanja wakamuumbua akapotea sana..kumbe kaibukia huko
 
Muda huu anaendelea kuhubiri hapa mtaani kwetu kuhusu Kanumba na Diamond kuwa ni ma 'freemason, tena anasema ana mafuta matakatifu kutoka kwa mungu ambayo atayatumia kuangamiza dunia anasema aliyaonyesha dah! Mji mzima ulipatwa na taharuki na kusema yeye ni nabii.

Ni kijana tu, amenyoa kiduku, t shirt lina mistari, ana suruali modo nyeupe amekuja na kagari kadogo ka 'kirikou' samahanini kwa kuandika bila mpangilio maana nipo kwenye msongamano wa watu.

Naomba mwenye taarifa za huyu mtu anipe

Chanzo: Mimi mhudhuriaji

Eneo: Dodoma, Bahi mission, eneo la Singidani
Nabii Kairuki..dah MUNGU atusaidie na hawa watumishi wa kisasa
 
Back
Top Bottom