Huyu mzee asipokuwa makini kuna siku atalia kilio cha mbwa.

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,774
3,460
Habari za wikiend wakuu..

Kuna mzee mmoja mfanya kazi mwenzangu lakini kwasasa amekua mtu wangu wa karibu kwa kila kitu.
Akiwa na shida labda ya kuhusiana na miamala anajaribu kujiweka wazi sana hadi namuonea huruma maana nahisi siku akifanya kwa mtu mwengine atamliza.

Ishu ni kwamba hajui kutumia mitandao vizuri hata fb nilimfungulia mimi na kumfundisha baadhi ya mambo lakini ni mzee wa kuhonga balaa.
Kinachonisikitisha ni kwamba akinambia nimtumie aidha dem wake pesa kupitia nmb mobile ikifika sehemu ya kuweka pin nampa aweke mwenyewe.. Lakini chakushangaza ananiambia niweke tu na hunitajia namba bila kujua kwamba hili ni tatizo.

Na ubaya wa mambo anakua mropokaji maana alinambia sasa kwenye account yangu kuna m 6 na upuuzi sasa hajui kama siku akikutana na tapeli analizwa? Ila sijawahi kumwambia lakini kuna siku kama sio leo nitamwelewesha asiwe mwepesi sana wa hayo.
Namba za siri aandike mwenyewe,.. mimi ningekuwa nataka kumfanyia wizi ningekuwa nishamliza zamani maana ananiachia sim yake na namba zote za siri nazijua anazotumia.

Namuonea huruma asije kupata mwanamke wa Dar akamliza akaja kupata aibu.. Hapa nnapoandika nipo nae na mda mfupi nitamweleza maana namtania sana.

==============================
UPDATES: Nilitoka kumweleza mda simrefu ila kakataa kwamba hafanyi hivo na na anaeijua ni mke wake pekee.. Sasa nimeamua kumpa uthibitisho nikamtajia zile namba akabakia kuduwaa ila kashukuru sana na pia kasema akifika atabadilisha nakuweka nyingine maana anatumia mwaka wake wa kuzaliwa.

Pia nimemshauri awe makini anapofanya vitu vyake asiwe msahaulifu sana itakuja kumletea shida. Nimemwelewesha kwamba ukipata mtu anaweza kuvizia sim yako na kukuibia pia awe makini na kutoatoa namba za siri hata za smart.

Kwakweli niliona kama kafadhaika kiasi kidogo baada ya kumtajia zile namba... Naamini haendi kubadili maana hajui hata jinsi ya kufanya si unajua kutumia smartphone uzeeni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom