Huyu mwanaume mimi namwacha

kwenye mapenz kikubwa ni uvumilivu ipo siku ataacha tabia hizo chamsing mvumilie tuu.
 

Mweh! na wewe unaongea sana bwana!
Haya ndiyo hivyo nishaamua kuachia ngazi nawapisha wengine.
 
inaonyesha jamaa atakua hana hela angekuanazo vituko vyote ungevumilia tu cc lara 1 LMAO

Ha ha ha ha ha haaaaa, huku kwetu visiwani si sawa na huko kwenu Bara, mapenzi ya pesa hayana thamani, ni upendo pekee ndiyo una nafasi
 
pole sana,,,,awali ni awali hakuna awali mbovu,halafu nimeona hapo jamaa alivotamani akupate kirahisi japo ktk mahusiano hutokea mengi kipindi cha kuachana na mwenza wako wa kwanza ukakimbilia chap kwa huyo dah sikukushaur kabisa hvi we hukosei halafu ukiachana na huyo utatafuta tena mwingine kwa style hiyo utadate na wangapi?? hvi ukimwacha ndo utakua umepata suluhu?


ukisha jibu hayo ntaja na mengine
 

kwa kweli mpendwa huyo si mwanaume, ukiingia kwenye ndoa unaweza usimalize mwaka ukatoka loh
 
alafu huwa najiuliza sana kwanini wanaume wengi ambao huwa marafiki wa kawaida kwa wadada wanapoanza mahusiano ya mapenzi hugeuke the worse bf ever? yani nimeshasikia wadada wengi sana wanalia na mahusiano ya aina hyo
 
mapenzi kizunguzungu

Dunia inayomambo, mambo yenye kuzidia,
Mambo kujaa vijambo, utaijua dunia,
Bora 'sifate mkumbo, mambo huleta udhia,
Mola naomba hekima, nikabili haya mambo.

Mola naomba hekima, ili niweze tulia,
Nifunze yaliyo mema, na si mtu kumwonea,
Mdomo usije sema, jambo sijafikiria,
Mola naomba hekima, nikabili haya mambo.

Mola naomba busara, iweze nitangulia,
Nisiifanye papara, mambo yanayonijia,
Unepushie hasira, kichwa kipate tulia,
Mola naomba hekima, nikabili haya mambo.

 
Jiweke pembeni kuepusha msongamano mwaya... Zinduna
 
Last edited by a moderator:
Zinduna....yako yanafanana na yangu....halafu jamaa wa huko huko Zenji...

Aise nimenyanyua mikono juu...kama ndo kupendwa ule upendo umenizidi umri....!
 
Zinduna,

Mpenzi wako wa kwanza sababu za msingi za kuwachana zilikuwepo, pole sana.

Ila huyu sioni sababu ya msingi hapo, Mwambie usiyoyapenda na unayoyapenda, kwa upande wako kuwa muwazi kwenye mawasiliano yako na simu, inaonekana kuna vitu haelewi kwenye mawasiliano yako na friends zako wa kiume na ukumbuke na yeye alikuwa rafiki yako wa kawaida pia na mawasiliano ndio yamewafikisha hapo!! unatarajia yeye ataamini kirahisi tu?

Hatutarajii wivu usiwepo kwenye mapenzi kabisa lakini swala la imani kwa mpenzi inategemea anavyo behave.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…