Huyu mwanaume mimi namwacha

Huyu mwanaume mimi namwacha

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
2,378
Reaction score
3,392
Naomba na miye leo nifunguke.

Nina mwanaume tumekuwa kwenye uhusiano kimapenzi (namaanisha kimapenzi) kwa takriban mwaka mmoja sasa. Lakini tulijuana miaka mitatu iliyopita akiwa kama rafiki mwema kwangu.

Ni kijana mwenye sifa nizipendazo, yaani ni mtaratibu, mwerevu, mwelewa, mwenye malengo na pia mcha Mungu.
Nilikutana na huyu kijana wakati wa tamasha la Mwakakogwa huko Makunduchi, basi kuanzia hapo tukawa marafiki. Aliwahi kunitamkia kuhusu kuwa na urafiki wa kimapenzi,lakini sikumkubalia kwa sababu nilikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine ambaye tulikuwa na malengo ya kufunga ndoa.

Kusema kweli nilivutiwa na huyu kijana ila nilishindwa kukubali kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi kwa sababu nilishaji commit kwa mwanaume mwingine, na miye ni binti niliyelelewa katika maadili kwa hiyo sikuwa tayari kumpaka mafuta huyu kijana wa watu kwa nyuma ya chupa, yaani kuwa mnafiki na ndumilakuwili wa kutaka huku na kule.

Urafiki wetu na huyu kijana ulikuwa ni wakawaida tu na mara chache tulikuwa tunakutana kwa mazungumzo ya hapa na pale katika kubadilishana mawazo.
Katika kipindi ambacho huyu mwanaume niliyekuwa naye nilipomfumania na shogangu wa kupika na kupakua wakiwa kitandani wakifanya tendo, nilimsimulia huyu kijana kama rafiki mwema ili kupata ushauri na pia kufarijiwa kwa sababu tulishakuwa marafiki kwa muda mrefu.

Alinishawishi sana nisivunje uhusiano na mpenzi wangu, akinisihi nimsamehe kwani ni ibilisitu alimpitia, lakini kutokana na kuumizwa na usaliti niliofanyiwa na mpenzi wangu niliyemuamini sana nilikata shauri niuvunje uhusiano na kushika hamsini zangu.
Nilikaa kwa muda wa miezi sita bila kuwa na uhusiano, lakini pia nilisita kuwa karibu na huyu rafiki yangu kwa muda wote huo nikitaka kutafakari kilichonitokea nikiwa peke yangu.

Yule kijana wala hakufanya makeke ya kunitafuta, na yeye alikata mawasiliano. Baada ya hiyo miezi sita ya kuachana na mpenzi wangu, nikarudisha mawasiliano na huyu rafiki yangu baada ya kukutana kwenye mkesha wa Maulid ya kuzaliwa Mtume. Baada ya kurudisha mawasiliano ndipo akanitaka tuanzishe uhusiano wa kimapenzi akiniahidi kwamba tutaoana iwapo kila mmoja ataridhika na tabia za mwenzake.


Tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi na nilijenga imani kwamba, huyu atakuwa mume mwema kwa sababu anazo zifa zote nizitakazo, na tulishafahamiana kwa takriban miaka miwili nyuma kama marafiki na kila mmoja alikuwa anafahamu kuhusu mahusiano ya mwenzake.

Kwa upande wake, yeye aliwahi kunisimulia kwamba alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa hajatulia, na hawaendani na hivyo aliamua kuvunja uhusiano huo.

Lakini baada ya miezi kadhaa tangu kuanzisha uhusiano na huyu kijana, na yeye akaanza vibweka. Kwanza ana wivu kupindukia, na anapenda sana kuzungumzia mahusiano yangu ya nyuma kwa namna ya kuniumiza kihisia. Wakati mwingine tukiwa kitandani anataka kujua ni nani mzuri zaidi kati yake na huyo bwanangu wa zamani katika swala zima la kitandani.


Hata nimsifie, lakini anahisi kama namnafiki tu na anapenda sana kusifiwa sifiwa na kudekezwa na kunithibiti nisiwasiliane na marafiki zangu. Hamuanini mtu yeyote wa jinsia ya kiume kuwa karibu na mimi, na hivi sasa anataka kuingilia mawasiliano yangu ya simu akitaka kujua nawasiliana na nani na kwa nini.

Kuna wakati aliwahi kufuta namba zote za wanaume niliowasevu kwenye simu yangu ambao wote ni jamaa zangu ambao nina nasaba nao.


Nimeshindwamiye, bora yeshe, mwanaume gani huyu asiyejiamini, hivi tu ni wapenzi akijanioa si atanigeuza mdoli wa kuniweka hapo asubuhi na akirudi jioni anikute hapohapo.


Nimeshindwa miye.
 
Zinduna hebu andika hii habari kwa mpangilio mzuri basi...

Weka paragraphs iwe rahisi kusoma kwa uzuri

Btw chapa lapa kama unaona umeshindwa kuvumilia wivu wa mpenzio
 
Tatizo ni kwamba inaonesha huyo kaka ameshakujua sana udhaifu wako tokea awali mkiwa marafiki..kwahiyo anahisi kama alikupata kwa hiyo njia, anahisi ni rahisi mwanaume mwingine kukuingia na ndo maana anakukimbizia marafiki zako wa kiume..na wivu pia unamsumbua sana na ndo maana anaingilia privacy zako za kwenye simu..cha msingi vunja ukimya uzungumze naye nà umwambie hiyo tabia huipendi.. maana hajakukosea ukisema umwache utaacha wangapi..maana kila mwanaume ana mapingufu yake#okybye..
 
Pole sana! ili kukushauri vinzuri unatakiwa ungeandika miaka yako, na uko wapi? na huyo mpenzi wako ana elimu kiasi ngani?
 
Tatizo ni kwamba inaonesha huyo kaka ameshakujua sana udhaifu wako tokea awali mkiwa marafiki..kwahiyo anahisi kama alikupata kwa hiyo njia, anahisi ni rahisi mwanaume mwingine kukuingia na ndo maana anakukimbizia marafiki zako wa kiume..na wivu pia unamsumbua sana na ndo maana anaingilia privacy zako za kwenye simu..cha msingi vunja ukimya uzungumze naye nà umwambie hiyo tabia huipendi.. maana hajakukosea ukisema umwache utaacha wangapi..maana kila mwanaume ana mapingufu yake#okybye..
charty huyu mwanaume habebeki na ni janga ka Boko Haram
Nishajisemesha mpaka basi. Ni mwepesi kuomba radhi, lakini habailiki.

Nitasubiri kama hatatokea mwanaume mwingine mwenye sifa angalau asilimia hamsini, bora nisiolewe
 
Last edited by a moderator:
Mpenzi tunmgo tata sana wengine wakisema wivu kipimo cha upendo wengine wivu huo ni kutojiamini.
Bana eeehhh kwangu mimi wewe ndo muamuzi.
 
wewe hujashtuka tu?tatizo ni mlango alioingilia hataki mtu mwingine aingilie hapo hapo!!umenielewa? rafiki zako wa kiume hataki hata awasikie because yeye amechaguliwa miongoni mwao
Thats normal a pyschological threat kwake na kama unampenda you know what hakipendi kwanini usimpe Guarantee anayoitaka? hapo mimi sijaiona significant problem ya kumuacha huyo jamaa labda ziwepo ambazo hutaki kutuambia
 
Pole sana! ili kukushauri vinzuri unatakiwa ungeandika miaka yako, na uko wapi? na huyo mpenzi wako ana elimu kiasi ngani?
Miaka inahusikaje hapa jamani
Kwa elimu wote tuna shahada ya elimu ya juu

Haya toa ushauri wako sasa
 
Mapenzi sio mabaya ila wapenzi ndio wanaongopa
 
wewe hujashtuka tu?tatizo ni mlango alioingilia hataki mtu mwingine aingilie hapo hapo!!umenielewa? rafiki zako wa kiume hataki hata awasikie because yeye amechaguliwa miongoni mwake
Thats normal a pyschological threat kwake na kama unampenda you know what hakipendi kwanini usimpe Guarantee anayoitaka? hapo mimi sijaiona significant problem ya kumuacha huyo jamaa labda ziwepo ambazo hutaki kutuambia

Ghubu na kudeka
Kwao ni mtoto wa kiume pekee na alilelewa akitukuzwa na kudekezwa
 
Back
Top Bottom