Huyu Mwanamke simuelewi

RoadLofa

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
1,347
2,957
Kuna Mwanamke mtaani ni anakaa jirani na nyumbani kwetu siku za mwanzo nilikuwa nikikutana naye dukani napokwenda kununua vitu ananichangamkia sana na kwenye kusalimiana ananiambia nikiwa napita kwao niende kumsalimia

Basi bhana baada ya siku kwenda kwenda nikamuomba namba yake ya WhatsApp nikawa namchombeza kwenye status na kuchat naye kidogo sana, na nikamgusia I'm so interested with her, akauliza for real nikamwambia ndio hakujibu tena kitu nikakausha sikuchat naye tena

Sasa leo bhana nimepita kwao baada ya kuniona ameniuliza mara mbili mbona nipo kimya sana akimaanisha WhatsApp, sasa nashindwa kumwelewa nipo kimya kivipi?

Wadau nahitaji ushauri wenu
 
Kuna demu mtaani ni anakaa jirani na nyumbani kwetu siku za mwanzo nilikuwa nikikutana naye dukani napokwenda kununua vitu ananichangamkia....
Una umri gani kwanza?! Anyways ngoja nikutafsirie. Huyo binti amekuelewa sana. Kitendo cha kukuona na kufikia kukuambia yupo interested ukamtembelee ilikuwa ni signal kukujulisha kuwa macho yake yapo kwako.

Kitendo cha wewe kumfuata ilikuwa ni acceptance gesture umempa kumwambia umekubali kumfukuzia (pursuit) na kumpa offer za kumfanya ajiskie vizuri. Sasa kuwa makini na mtoto wa watu kama umemuona yupo vizuri kuwa wako usimharibu akili na michezo ya kijinga.

Sasa fanya hivi. Tafuta pesa kidogo hata 30,000 tu mwambie kwa kumshtukiza nataka nikutoe out luch. Mpeleke migahawa ipo mingi sana ya kwenda na watoto wa kike wakafurahia. Mtreat na hiyo offer ya lunch kisha mrejeshe kwao salama kama ulivyomchukua. Kisha muage na busu la utosi bila kumuomba. Kisha muage ondoka usiseme kitu chochote.

Ukifika home mnunulie bundle hata ya 2000 ya internet kisha mtakie mchana mwema.

Halafu utakuja kunambia hapa huyo binti kama atakuletea story za hawa wadangaji.

Kwa kifupi umependwa jiweke hapo kama umemuona yupo vema. Huku nje sio pazuri hawa mavampire (wadangaji) wamecharuka na wamevurugwa sisi matycoon huwa ndio tunawamudu kucheza na psychology zao ila hawana mahaba ya kweli yakiona damu (pesa) yanakusogelea yakunyonye yote iishe.
 
Una umri gani kwanza?! Anyways ngoja nikutafsirie. Huyo binti amekuelewa sana. Kitendo cha kukuona na kufikia kukuambia yupo interested ukamtembelee ilikuwa ni signal kukujulisha kuwa macho yake yapo kwako...
🙏bro kwa ushauri naufanyia kazi
 
Una umri gani kwanza?! Anyways ngoja nikutafsirie. Huyo binti amekuelewa sana. Kitendo cha kukuona na kufikia kukuambia yupo interested ukamtembelee ilikuwa ni signal kukujulisha kuwa macho yake yapo kwako...
Niliitumia ni njia nzuri sana
 
Kuna Mwanamke mtaani ni anakaa jirani na nyumbani kwetu siku za mwanzo nilikuwa nikikutana naye dukani napokwenda kununua ...
Nikiacha kukuuliza umri, nikuulize unachomiliki chenye kuonekana katika jamii, mf: duka ama biashara nyingine yoyote ile, una kazi yenye kuheshimika?

Haujawahi mfanyia vitimbi ama dhulma yoyote ndugu ama rafiki yake?

Upo smart kwa turn out yako, yaani upo soap soap unajipenda?

Moja wapo ya sifa kwa maswali niliyokuuliza, yaweza kukupa thamani ya mwanamke kujilengesha, kwa heri ama kwa shari.

Si kila jino unalokenuliwa usidhani ni la upendo, maana hata hasidi aweza kukufanyia hivyo ili kuficha hila ovu moyoni mwake.

Nashauri kama umempenda, mtongoze dhahiri ili upate msimamo wake uweze kupima mustakabali halisi.

Kama atakuwa alikutega kimaslahi hapo ndipo utakapomgundua baada tu ya makubaliano, maana "demand" zitaanza kumwagika.

Sitaki kusikia unajihusisha na mke wa mtu.
 
Kuna Mwanamke mtaani ni anakaa jirani na nyumbani kwetu siku za mwanzo nilikuwa nikikutana naye dukani napokwenda kununua vitu ananichangamkia sana na kwenye kusalimiana ananiambia nikiwa napita kwao niende kumsalimia
Nipe namba yake, nitamuuliza alafu nitakujibu PM
 
Back
Top Bottom