Dah, mkuu naona kama wewe ndiye mwenye matatizo hapa.
1. Unaonesha bado hujakubaliana na maelezo yake juu ya kilichotokea kuhusu mtoto. Hivyo, ingawa humuambii, lakini moyoni mwako unajua huna amani wala imani kubwa ju yake.
2. Ngono ni kitu kimoja powerful sana. Kilimuangusha hadi mfalme Daudi. Ukifanya ngono na mtu kuna maamuzi mengine baadaye ukija kuyawaza huamini kama uliyafanya. Dunia ya sasa imefanya ngono kuonekana kuwa kitu cha kawaida (kuingizia na kutoa) lakini kiuhalisia ni very powerful. Kama utaweza, mkae walau mwezi (ningependekeza ile formula maarufu ya siku 90) bila kufanya ngono. Muishi kawaida na kushirikiana mambo mengine. Kama baada ya siku hizo 90 utajisikia bado unampenda na kumhitaji basi tutahamia point ya 3.
2 (b). Kama ukigundua upo naye kwa kuwa ni mzuri wa sura na umbo na kwamba yupo tayari kwa ngono kila unapomhitaji then naamini unajua cha kufanya. Hiyo pia itasaidia kujua kinachokupa hesitation huenda ni ile 'nimemzoea' tu na si upendo kama ambavyo unajiaminisha.
3. Ukigundua kuwa unampenda kweli na mnaweza kuishi pamoja na kupanga na kufanya mengine bila kuwa na kiunganishi cha ngono, basi fanya jambo la busara ambalo naamini ungependa dada zako wafanyiwe. Nenda kamchumbie mfunge ndoa. Muoneshe unamthamini. Kisingizio cha kusema mtoto wa kwanza hukumpata ndani ya ndoa hakitosi kuhalalisha yeye kushika mimba yako sasa. Wanasema kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa. Kila siku tunaimba hapa kuwashauri single mothers kutorudia hayo (hapa nakumbuka maushauri tunayompaga dada mmoja anajiita
Anna pita ). Kama kweli unampenda, umepata amani ya yote yaliotokea na hutokuja kuyatumia baadaye kumuumiza (ni muhimu sana upate amani ya moyo juu ya haya) basi fanya hima mfunge ndoa. pamoja na kwamba dini zinatutaka hivyo lakini kisheria itamlinda yeye na watoto.
4. Hili jambo nimelifikiria leo wakati nawaza ya kwangu. Ndoa ni jambo la ajabu sana. Yani unaondoka kwa watu uliounganishwa nao kwa damu (mama yako) na kwenda kuishi na mgeni (mkeo) na tena anakuwa na priority kuliko mama yako wa damu. Ni fumbo ambalo nimewaza nikakosa jibu. Lakini point yangu ni, unapofanya uamuzi huo (kama ni wa imani basi omba sana) jua ni uamuzi unaotakiwa 99% uwe ni mawazo yako peke yako. Ukichanganya ushauri wa watu juu ya nani uwe naye hamtofika mbali. Simaanishi upuuze ushauri wa mama yako lakini jitahidi sana kufanya maamuzi yako. Hata ukimuacha huyu.
5. Hii nimarudio lakini nadhani ni ya muhimu kuisema tena. Maelezo yako yanaonesha bado una 'reservations' juu ya binti. Bado una kusitasita juu yake, maelezo yake na huna amani 100%. Jitahidi sana kabla hamjapeana mimba uwe umesuluhisha hili moyoni mwako. Umewaficha ndugu na wazazi juu ya mtu unayetuambia unampenda. Mimi hapa naona red flag kubwa mno...ni vile nikiandika zaidi utachoka kusoma.
MWISHO nisaidie kumpa hongera huyo binti kwa kuweza kujilinda asishike mimba ya pili kabla ya ndoa. Kwake ndoa ni muhimu ila inaonesha kwako haina uthamani wowote (sikuhukumu though). Ila mpe hongera zangu na ukiweza muambie akuepuke mpaka pale ambapo definition zenu za maisha (hasa ndoa kwa hapa) zitakapofanana.