Dada hakuna kitu kibaya kama kuvunja ndoa, inabidi uwe na uhakika asilimia mia kwamba wewe haukusababisha migogoro kwenye nyumba yako. Ningekuwa mimi ni wewe, maadam kutokuelewana kwenu hakujahusisha vipigo, ningekaa chini na mume wangu nimueleze nia yangu ya kutofanya nae mapenzi mpaka hapo atakapotulia na tukapima, ningeishi nae vizuri ila tu mambo ya unyumba ni mpaka atakapobadilika, Hata akirudi asubuhi we mwambie karibu mme wangu wala usigombane kwamwe ugomvi haujengi, ningeishi vizuri na hao watoto wake kwani hiyo ndio sababu ya kujivunia kuwa mama bora, hazina yako ya baadae, furaha yako na baraka zako zote zitapitia hapo. Bado unaweza fanya biashara zako ukiwa na huyo mumeo sasa hivi kwani atakukataza?? Sikushauri kuondoka, do something....