Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 14,510
- 27,003
Hakuna cha salamu!
Kumekuwa na hii kasumba ya kujibu maswali ya watoto wetu wanapodadisi kuhusu upatikanaji wa 'wadogo' zao, mtoto akihoji anataka mdogo wake ataambiwa “nitaenda kununua” nikuletee!
Naye basi anafurahia ahadi na hata mdogo wake atapopatikana basi hutamba kuwa mama yake amemnunulia, kwanza ni nini msingi wa uongo wa namna hii?
Basi turudi kwenye hoja.
Ni sahihi kuwaongopea watoto mambo ya kikubwa kwa kisingizio cha umri wao?
Kama uliwahi kuwa mtoto, huenda uliwahi kudanganywa hivi pia. Kama una kumbukumbu nzuri, uligundua ukweli [kwa njia gani] ukiwa na umri gani?
Wazazi wengi kwa sababu mbalimbali wamekuwa hawawezi kuzungumza na watoto wao kuhusu elimu ya uzazi, watoto wanakua tu na kujikuta kila mmoja anaelewa kwa namna yake.
Je, kama kuna haja ya kuzungumzia hili... upi ni umri sahihi kwa mtoto kupewa elimu hii?
Wasalaam.
Ncha Kali.