Huyu msichana mimi simuelewi

Kumbe tuko wengi tunaumizwa kwa design hiyo. Mimi ilishawahi kunitokea nikaamua kutulia kama maji kwenye mtungi. Siku zikapita, wiki, mwezi, miezi hata miaka. Hivi karibuni nimekutana naye. Kwanza it was a surprise, hakuna aliyetarajia kama tungeonana maana na namba za simu tulishapotezana. Aisee, utamhurumia binti amechoka maisha yamemgonga kisawasawa. Alafu mimi mambo swafiiiiiiiiii, nilimsalimia akaniomba namba nikampa sikutaka hata kupiga naye story, nikaingia ndani ya gari langu nikafunga kioo huyooooooooo. Akanitafuta kwenye simu nikawa nampa dry mpaka alilia machozi. Nikamwambia its too late mama, am somebody's husband and with kids. Sikumpa hata hela ya vocha nyambafu
 
Usimpe nafasi ya kujitetea,huyo ni msaliti tu na kamwe awezi kubadilika,chamsingi wewe mpotezee tu,heshimu uamuzi ulionao sasa
 
Ukiwa muongo uwe na kumbu kumbu , ww si ndo umeandika thread nyegine km hii na kudai alikuomba 50000 mara tena hii unasema 200000 hemu sema mkuu ukwel tutaelewa
 
bahati nzuri nilipata ambaye ananipa viti el-mubasher hadi nimerudi kuwa kama captein komba
huyo wa sasa hivi hakufai kiafya mrudie yule yule wa mwanzo ndio anajua kupunguza uzito wako
 
Usimjibu text kabsa wala kuhangaika kumtafta..muache ahangaike kuktafuta mwenywe akikupata mskilize anayoongea alaf muitkie ok,tembea zako
 
muepuke hakufai huyo muepuke kama ukoma amemiss hela zako tu au msikilize mpe shsrti la kutokupiga mzinga hadi muish wote
 
mkuu mi naomba utupe mrejesho!natamani kujifunza kitu kupitia hili tukio!
 
Usiwasiliane nae huyo maana unaweza kumhurumia
 
Usiwasiliane nae huyo maana unaweza kumhurumia

Ameshachuja mkuu, sasa hivi siwezi. Wazuri wanazaliwa kila siku... bahati haiji mara mbili. Unajua tatizo moja wadada hawajifunzi. Wanashindwa kutofautisha mwanaume serious wa maisha na mwanaume wa starehe. Bahati mbaya wa starehe kwa wakati huo anaonekana kujali sana kuliko aliye serious na maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…