Huyu mke wa mtu ananitafutia matatizo!

Huyu mke wa mtu ananitafutia matatizo!

Mfalme Akili

Member
Joined
May 28, 2017
Posts
88
Reaction score
55
Habari zenu ndugu,

Nakumbuka kwa mara ya kwanza nilikuja humu JF kuomba ushauri katika jambo lililonitatiza kwa wakati ule na kweli wana JF walinishauri na ushauri ulinisaidia na kwa sasa niko poa.

Leo nimekuja tena na jambo hili linalonitatiza naomba ushauri wenu nifanyeje!

Kuna binti nilisoma nae O-level miaka kadhaa iliyopita na tukapotezana kwa miaka mingi lakini kwa vile milima haikutani ila binadamu hukutana basi tulikutana miezi kadhaa liopita kwenye harusi ya jamaa yangu mmoja hivi.

Ki ukweli kwa vile tulipotezana miaka mingi hata hatukua na mawasiliano hivyo tulipokutana tulifurahi sana kwa vile tulikua marafiki sana enzi za O-level na nakumbuka nilimtongoza kipindi kile akanikataa kabisa hivyo tukawa ni marafiki wa kawaida tu, baada ya kumaliza O-level tulikua katika contact ila baada ya miaka kadhaa kupita akawa hapatikani kwenye namba yake na mimi kuna wakati ilifikia nikabadili namba hivyo tukawa tumepotezana rasmi! Hivyo baada ya kukutana tulifurahi tukakumbushana enzi zile na kuelezana our current situation kisha tukabadilishana namba. Moja ya vitu alivyoniambia ni kua kwa sasa keshaolewa na ana mtoto mmoja. Basi nikampa hongera kisha tukaachana siku ikapita.

Siku iliyofuata alianza kunichatisha akiniulizia mke wangu na watoto, nikamjibu ki ukweli bado sijabarikiwa kuoa ila nilikua na mchumba aliyenisaliti sana na nimeachana nae si kitambo sana hivyo kwa sasa bado sijaingia tena kwenye commited relaltionship. So tukachati ila kilichonishangaza akaniambia anahitaji tuonane sehemu tuongee zaidi basi na mimi nikamkubalia.

Jioni tukakutana kwenye hoteli fulani aliyoipendekeza yeye, tuliongea mengi ila akaniweka wazi kua mambo yake kiuchumi si mazuri kama nina weza kumsaidia apate kazi atashukuru sana, na mimi nikamwambia nitajitahidi, basi tukaachana siku ikapita. Ila kuanzia siku hiyo akawa ananichatisha sana na simu kila mara, mara anakumbushia nilivyomtongoza akanikataa na kusema ule ulikua utoto n.k. basi tunacheka na kutaniana.

Kuna siku akaniambia ana shida na nimkopeshe kiasi flani cha hela, basi na mimi kwa vile nilikua nayo nikampatia. baada ya siku kadhaa kupita akaniambia tena kua amekwama nimsaidie kiasi fulani cha hela, kumbuka hapa lugha haikua nimkopeshe hapa alisema anaomba, basi na mimi nikatoa kwa vile nilkua nacho. Siku zikapita akaanza kunisimulia matatizo ya mumewe sasa mimi kama mwanaume sikupendezwa na hilo nikamwambia unaponiambia kua mumeo haudumii familia ni kumdhalilisha so usimfanyie hivyo but akawa hajali, sasa mara akaanza kuniomba hela za salon, mara mtoto wake amepungukiwa ada nimsaidie basi mimi nikawa natoa ninapoweza kwa upendo tu.

Ila sasa nikaanza kujisikia vibaya kwa sababu mda mwangine ananiambia dhahiri jinsi anavyomchukia mumewe na kila udhaifu wa mumewe anaumweka bayana na hadi mda mwingine ananiomba hela ya matumizi nyumbani. Sasa kuna siku nimemwambia mumeo hua hakuulizi unatoa wapi fedha hizi, akajibu kua hawezi kumuuliza coz anajua kua anajishughulisha na vikoba.

Sasa kilichofanya niandike uzi huu ni kwamba huyu binti amenitamkia kabisa kua anataka aachane na mumewe ili awe ana mimi, nikamuuliza kwanini ufanye hivyo? akajibu eti jamaa hawezi kumhudumia yeye na mtoto wake! nimejisikia vibaya sana kwani mimi nimekua nikimsaidia kwa upendo kama rafiki ila kwa sasa amekua akiniomba hela kama vile mimi mumewe na kunitaka kimapenzi.

Kwa jinsi nilivyosalitiwa najua ni jinsi gani inauma mke wako kuliwa na mtu mwingine, na hapa nikiangalia kigezo kikubwa kwanini huyu binti anafanya hivyo ni kwa sababu jamaa ana hali ngumu kimaisha.

Hivyo naomba ushauri wenu maana nimetamani kukata mawasiliano nae ila kuna siku kanipigia simu kua mtoto wake anaumwa sana yuko hospital but amepata changamoto ya fedha, ikabidi niende hospital kuhakiki nikawakuta kweli, na mtoto alikua amedhoofu sana, ikabidi nimsaidie.

Sasa nawaza nikiendelea kumsaidia anakua ananitaka niwe nae kimapenzi na nikisema nikate msaada nakua namuonea huruma mtoto, na ki ukweli jamaa ambae ni mumewe yupo katika wakati mgumu sana coz amepoteza ajira yake na bado hajapata ajira.

Je nifanyeje? Maana sitaki kumlia jamaa mke wake, but as long as naendelea kuwasiliana na huyu mwanamke ni kwamba anafanya mazingira ya mimi kua kama mume wake na anaushawishi mkubwa ki ukweli maana ni mrembo sana.

Asanteni.
 
Huruma huponza. Achana nae kama anataka kuachana na jamaa yake kisa maisha magum, ipo siku na wewe atakufanyia hivyo hivyo. Mwambie umesharudia na demu wako
 
Anhaa unataka kuwa MATALA?( mke wa pili wa jamaa) ndugu wema ukizidi sana, utajiharibia, achana na mke wa mtu ndugu, naiusia nafsi yangu pamoja na kuiusia nafsi yako, chonde chonde ndugu...sa hizi vyuma vimekaza usiwatafute watu ubaya
Dunia hii ione tu hivi, wema wangu huu unanipeleka pabaya
 
Tatizo la mwanamke ukimsaidia sana anajua unampenda.
 
Huyo mkimbie, kimbia sana ndugu yangu usijeuke nyuma!! Huyo ana roho mbaya zaidi ya mkaanga sumu!!

Anataka kumwacha mumewe kwa kuwa hana hela na wewe siku ukiishiwa atakukimbia..
Yani kumuepuka yule labda nibadili namba zangu za simu,
 
Hili nalo lakushinda mkuu, kaa nae mbali.... Tena mbali kabisa, kabla hamjaonana alikuwa aishije labdaa.... Huyo kakupendea fedha kama Huamini anza kumdanganya Uchumi wako umeyumba na hali ni mbaya kama hajakimbia!!!!
 
Achana naye na mwambie ukweli kuwa yeye in mke wa MTU, pia kumbuka hata wewe itokee umekosa pesa ya kumuhudumia basi ataenda kwa mwingine tena.
 
Tatizo la mwanamke ukimsaidia sana anajua unampenda.
Umeona eh, watu wengine tumesaidiwa sana na tumepitia maisha magumu hivyo mtu akiwa na tatizo moyo unakusuta usipomsaidia, lakini mtu anapotumia hiyo kama advantage is not fair kabisa.
 
Back
Top Bottom