Huyu mke wa mtu ananitafutia matatizo!

Habari zenu ndugu,

Nakumbuka kwa mara ya kwanza nilikuja humu JF kuomba ushauri katika jambo lililonitatiza kwa wakati ule na kweli wana JF walinishauri na ushauri ulinisaidia na kwa sasa niko poa.

Leo nimekuja tena na jambo hili linalonitatiza naomba ushauri wenu nifanyeje!

Kuna binti nilisoma nae O-level miaka kadhaa iliyopita na tukapotezana kwa miaka mingi lakini kwa vile milima haikutani ila binadamu hukutana basi tulikutana miezi kadhaa liopita kwenye harusi ya jamaa yangu mmoja hivi.

Ki ukweli kwa vile tulipotezana miaka mingi hata hatukua na mawasiliano hivyo tulipokutana tulifurahi sana kwa vile tulikua marafiki sana enzi za O-level na nakumbuka nilimtongoza kipindi kile akanikataa kabisa hivyo tukawa ni marafiki wa kawaida tu, baada ya kumaliza O-level tulikua katika contact ila baada ya miaka kadhaa kupita akawa hapatikani kwenye namba yake na mimi kuna wakati ilifikia nikabadili namba hivyo tukawa tumepotezana rasmi! Hivyo baada ya kukutana tulifurahi tukakumbushana enzi zile na kuelezana our current situation kisha tukabadilishana namba. Moja ya vitu alivyoniambia ni kua kwa sasa keshaolewa na ana mtoto mmoja. Basi nikampa hongera kisha tukaachana siku ikapita.

Siku iliyofuata alianza kunichatisha akiniulizia mke wangu na watoto, nikamjibu ki ukweli bado sijabarikiwa kuoa ila nilikua na mchumba aliyenisaliti sana na nimeachana nae si kitambo sana hivyo kwa sasa bado sijaingia tena kwenye commited relaltionship. So tukachati ila kilichonishangaza akaniambia anahitaji tuonane sehemu tuongee zaidi basi na mimi nikamkubalia.

Jioni tukakutana kwenye hoteli fulani aliyoipendekeza yeye, tuliongea mengi ila akaniweka wazi kua mambo yake kiuchumi si mazuri kama nina weza kumsaidia apate kazi atashukuru sana, na mimi nikamwambia nitajitahidi, basi tukaachana siku ikapita. Ila kuanzia siku hiyo akawa ananichatisha sana na simu kila mara, mara anakumbushia nilivyomtongoza akanikataa na kusema ule ulikua utoto n.k. basi tunacheka na kutaniana.

Kuna siku akaniambia ana shida na nimkopeshe kiasi flani cha hela, basi na mimi kwa vile nilikua nayo nikampatia. baada ya siku kadhaa kupita akaniambia tena kua amekwama nimsaidie kiasi fulani cha hela, kumbuka hapa lugha haikua nimkopeshe hapa alisema anaomba, basi na mimi nikatoa kwa vile nilkua nacho. Siku zikapita akaanza kunisimulia matatizo ya mumewe sasa mimi kama mwanaume sikupendezwa na hilo nikamwambia unaponiambia kua mumeo haudumii familia ni kumdhalilisha so usimfanyie hivyo but akawa hajali, sasa mara akaanza kuniomba hela za salon, mara mtoto wake amepungukiwa ada nimsaidie basi mimi nikawa natoa ninapoweza kwa upendo tu.

Ila sasa nikaanza kujisikia vibaya kwa sababu mda mwangine ananiambia dhahiri jinsi anavyomchukia mumewe na kila udhaifu wa mumewe anaumweka bayana na hadi mda mwingine ananiomba hela ya matumizi nyumbani. Sasa kuna siku nimemwambia mumeo hua hakuulizi unatoa wapi fedha hizi, akajibu kua hawezi kumuuliza coz anajua kua anajishughulisha na vikoba.

Sasa kilichofanya niandike uzi huu ni kwamba huyu binti amenitamkia kabisa kua anataka aachane na mumewe ili awe ana mimi, nikamuuliza kwanini ufanye hivyo? akajibu eti jamaa hawezi kumhudumia yeye na mtoto wake! nimejisikia vibaya sana kwani mimi nimekua nikimsaidia kwa upendo kama rafiki ila kwa sasa amekua akiniomba hela kama vile mimi mumewe na kunitaka kimapenzi.

Kwa jinsi nilivyosalitiwa najua ni jinsi gani inauma mke wako kuliwa na mtu mwingine, na hapa nikiangalia kigezo kikubwa kwanini huyu binti anafanya hivyo ni kwa sababu jamaa ana hali ngumu kimaisha.

Hivyo naomba ushauri wenu maana nimetamani kukata mawasiliano nae ila kuna siku kanipigia simu kua mtoto wake anaumwa sana yuko hospital but amepata changamoto ya fedha, ikabidi niende hospital kuhakiki nikawakuta kweli, na mtoto alikua amedhoofu sana, ikabidi nimsaidie.

Sasa nawaza nikiendelea kumsaidia anakua ananitaka niwe nae kimapenzi na nikisema nikate msaada nakua namuonea huruma mtoto, na ki ukweli jamaa ambae ni mumewe yupo katika wakati mgumu sana coz amepoteza ajira yake na bado hajapata ajira.

Je nifanyeje? Maana sitaki kumlia jamaa mke wake, but as long as naendelea kuwasiliana na huyu mwanamke ni kwamba anafanya mazingira ya mimi kua kama mume wake na anaushawishi mkubwa ki ukweli maana ni mrembo sana.

Asanteni.
Huenda wewe ndiyo chanzo cha huyo mdada kuzidi kumchukia mume wake, jiepushe nae mbali dhambi ya kuitenganisha ndoa yao itakutafuna na haitakuacha salama, mweke wazi hupendi na hutegemei kuwa katika mahusiano nae..wewe mwenyewe unaomba ushauri lakini tayari umeshatamani kupindua ndoa ya watu unasubiri majira tu, maana unamsifia mzuri kua makini sana na unachotaka kufanya.....
 
Unajaribu sumu kwa kuionja mkuu? Achana na vya watu pia huyo mwanamke sio tu hafai kuoa bali hata kulala nae kwa usiku mmoja jiangalie siku atakupeleka kibra ilimradi apate pesa!
 
Mkuu mbona we mwenyewe una majibu!
Unavyoendelea kuwa karibu na huyo mwanamke ndio utazidi ku create nafasi za kuzini nae hata kama ulisha apa kutomtendea mwanaume mwenzio hivyo!
Mke wa mtu sumu kaka!Nakuhakikishia siku mumewe akijua kuna mtu anamwezesha mkewe kwa sababu eti yeye yuko ktk kipindi kigumu financially,ndio utajua hasira ya maskini!Labda nae awe yule wa kulelewa!
 
Huyo jamaa aliemuoa ndio alikuwa chaguo lake shenzi type. Leo hii kafulia anamuona kituko sio! Hapo kaza uzi huyo mwanamke ana akili ndogo ambazo hazijazi hata kisoda.

Usikubali akurubuni yeye ni mke wa mtu anatakiwa alieheshimu hilo no matter what atafte namna ya kusaidiana na mumewe tu.

Namuonea huruma jamaa nahisi ni mmojawapo wa majipu yaliotamba enzi za mkwere governance na kwa uhakika ule dili za mipesa na ajira akaamua abebelee mwanamke mrembo sana mwenye tako asijue kuwa kinachodumisha upendo ni akili, utu na uvumilivu wa mke kipindi cha majanga!
 
Jua kutoka kwake kuwa ana mpango au mkakati gani wa kuendesha maisha ya familia yake, na sio kuja kuwa mzigo kwako. Kama Ana mipango wa kufanya biashara, msaidie mtaji na iwe ni mwisho wa wewe kuwa na mawasiliano naye. Ujitoe kabisa katika maisha yao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom