Kenya wamepitisha sheria ndogo ya kucontrol makato ya kodi kwa kipato wanachokipata watumishibwa mungu. Maana imekuwa ni fashion trendy sasa kila mtu kukodi ukumbi na vyombo vya muziki kupiga injili na kujinasibu kama ni mpakwa mafuta wa bwana ama nabii refer to dsm kuna manabii karibu 200. Wengine ni wahamiaji haramu wapo toka rwanda anakuja anazamia kahama huko miaka kadhaa anajifunza kisukuma anakuja mjini anapanga eneo na kutangaza neno akiwa na lengo la kutajirika.
Mfano mchngaji mpaka ana marange rover halafu halipi kodi hii ni dhuluma sana. Sijawahi kusikia nabii fulani anasomesha watoto yatima mpaka university kwa pesa yake mfukoni anayochangisha waumini. Wengi wanakuja na michango ya kugharamia ujenzi wa kanisa,vyombo vya muziki,chekechea,shule za sekondari huwezi wasikia muumini anaumwa tumchangie hata siku moja au kakosa kodi ya nyumba tumchangie. Imefika wakati hawa watu wapewe efd machines kila mchango unaotolewa basi ukatwe kodi ni wachumia tumbo