Mtego wa Noti
JF-Expert Member
- Nov 27, 2010
- 2,591
- 1,599
ITV leo asubuhi kuna mgeni wamemualika anazungumzia mambo ya mapunduzi ya uchumi, kila baada ya sekunde anamtaja Kinana eti ni mwanamapinduziwa uchumi kwa kuwa amezungumzia tu kufufua kiwanda cha kubangu korosho huko Lindi. Anachoongea mpaka muda mwingine nakuwa simwelewi kabisa. Yaani mwanasiasa kuongea tu kuwa kiwanda cha korosho kifufuliwe basi ashakuwa mwanamapinduzi wa uchumi?
Kama hawa ndio wachambuzi mnaowaleta hapo ITV basi jiangalieni sana maana akiulizwa hiki anajibu kile mpaka wasilizaji tunakuwa hatujui anachokizungumzia. Kamfagilia huyo kinana mpaka sasa inakuwa kero maana binafsi sijaona alichokifanya kinana.
Poleni sana ITV najua mnapata tabu na huenda mngependa kipindi kiishe!