Nipo hapa naangalia sherehe za Mei mosi lakini nashindwa kuelewa huyu mshereheshaji ana matatizo ya kufikiri au ndio kujipendekeza kwa mkuu mpaka anaongea kauli zisizopendeza? Kwanza nilimsikia anawakemea watu kuwa "Tulieni kama mnafanyiwa tohara" nikadhani amepitiwa tu lakini amerudia tena kwa kumwambia mgeni rasmi kuwa "usiwe na wasiwasi hii mvua haitonyesha nina uwezo wa kuizuia" hapa amenishangaza sana, ina maana yeye ni Mungu au ni bingwa wa ushirikina? Sifa nyingine sio nzuri kuzitafuta kwenye halaiki kama hii.