Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,180
- 24,798
Mwanzoni wakati huyu kocha anapewa hii timu alishangiliwa kwa vifijo na nderemo na kuonekana kuwa huyu ndiye kocha aliyestahili kuichukua hii timu!
Alifanya usajili wa nguvu tena taratibu taratibu huku akidai kuwa anatafuta wachezaji makini wanaojua kucheza na namba zao vizuri ili kuhakikisha ubingwa unabebwa!
Mechi za mwanzoni kocha aliona kuna wachezaji wa zamani waliojulikana kama majipu walioonekana kutokucheza vizuri na namba zao, hao waliondolewa kwenye kikosi na namba zao kuchukuliwa na wachezaji wapya, wachezaji wa zamani waliobakia walihamishwa namba zao, golikipa akawa forward, washambuliaji wakawa mabeki yaani timu haieleweki maana huyu kocha hata kozi ya ukocha hakupitia na hata washauri wa timu hakubaliani nao!
Sasa timu imeanza kushiriki ligi, kila mechi kiwango cha timu kile tulichoaminishwa hakionekani!
Mashabiki wameamua kususia kuishabikia timu, wale wafadhili nao wengi hawataki kuifadhili timu.
Ilitokea hivi majuzi timu ilipatwa na mtikisiko wafadhili na mashabiki wakajitolea kuifadhili timu , lakini michango yao kocha akaelekeza isitumike kwa ajili ya walengwa!
...Huyo kocha amekuwa na lugha za kuudhi kwa mashabiki bila kujua wengi wao ndio waliopendekeza aletwe kwenye timu hatimae akapigiwa upatu na kukabidhiwa timu ili ainoe!
Hivi sasa timu inazidi kuporomoka siyo kwa kiwango, mapato, mashabiki na hata wafadhili!
......Hii timu isahau ubingwa, na wakuipandisha daraja itakuwa shughuli kweli kweli!!