Huyu Jamaa yangu Anamtongoza Mpenzi/Mchumba wangu ilhali kaambiwa ana mtu!

Zamani kidogo pale magomeni kulikuwa na Mpemba mmoja anafanya biashara ya kuuza vipande vya pweza mida ya jioni hivi, alipofikisha kiwango flani cha faida akaamua kufunga safari hadi Pemba na kuoa msichana mmoja toka kijijini kwao mrembo balaa. Baada ya upepo wa Dar kumkolea yule dada uzuri wake sasa ulianza kuonekana na kila mtu wenyewe wanaita natural beauty, she was very beautiful, kumbe pale pembezoni kuna kijana mmoja alimiliki taxi kadhaa alimuona na akawa anamtongoza daily, dada akaenda kumshatikia mume kuwa nikija hapa jioni kufata hela za mkate kuna jamaa ananitongoza daily, muuza pweza alimfata jamaa na akamuonya dhidi ya mke wake, jamaa anaemiliki taxi akatoa bomba akamwambia jamaa ukinizingua nakumaliza sasa hivi, muuza pweza kafunga duka kaenda pemba kufata kombora la kichawi, hadi ninavyoandika hapa jamaa mwaka wa 5 huu yupo kitandani na hospitali zote zimeisha. Sikushauri utafute kombora broo TheMason lakini ongea nae huyo kaka kwa wema na huenda akakuelewa.
Asantee saana!
 
umenikumbusha yule kijana..
alikua kila akinifuata na kueleza ombi lake namjibu nna mtu wangu
kila siku ni jibu hilohilo
uzalendo ukamshinda siku hiyo akanifungukia..kila siku jibu ni hilo nna mtu wangu..nna mtu wangu...kwani mi jini?
 
umenikumbusha yule kijana..
alikua kila akinifuata na kueleza ombi lake namjibu nna mtu wangu
kila siku ni jibu hilohilo
uzalendo ukamshinda siku hiyo akanifungukia..kila siku jibu ni hilo nna mtu wangu..nna mtu wangu...kwani mi jini?
Hahahaaaaa
 
Kuwa na mchumba ni jambo moja na kuwa na mke ni jambo jingine. Itoshe tu nikufahamishe kwamba mchumba si mke. Ni sawa na dereva anayeendesha gari bila kuwa na leseni na mwenye leseni anaweza kutoka nyuma akaajiriwa na kukabidhiwa gari.

Kwa msingi huo uchumba ni makubaliano ya muda kati ya watu wawili wenye nia ya kuoana na si ndoa kamili.
 
Acha kuamini anachokwambia mwanamke huenda anataka kuwachonganisha. Anakwambia kuwa kamwambia yupo na wewe ila jamaa haelewi je, una uhakika gani kuwa kamwambia yupo na wewe? Acha kuletewa we mwanaume, mfate jamaa muulize na umwambie yule manzi mkoje nae na akikataa ndo ujue cha kufanya japo magereza milango iko wazi.
NB: Msichana asiwe chanzo cha kuwakosanisha.
 
wakuu nisaidieni kuna huyu jamaa nafahamiana nae kama mshikaji mtaani sasa kuna manzi mmoja wa mtaani kwao nmebahatika kuwa nae mimi!

tatizo linakuja pale binti ananisumbua kwamba jamaa anamtaka....nimejaribu kumwambia binti amalize hayo mwenyewe ila anahitaji msaada wangu maana kamwambia jamaa kwamba ananipenda ila mchizi haelewi!

imefikia hatua jamaa ananichafua jina kwamba nina wanawake wengine na kwa status yangu mimi siwezi kuwa na priority na mwanamke kama yeye!

nimejaribu kupotezea ila nahisi itakula kwangu maana huyu mwanamke nina malengo naye sasa wadau Nishaurini serius je kwenye hali kama hii nichukue maamuzi gani nisikosee?

Ni ishu siriaz tafadhali!
kidonda bila inzi sio kidonda tena
 
Dah...acha ubwege Dogo... Unategwa...anajipandisha thamani ili ufanye maamuzi....wastani mwanamke anayevutia hutongozwa Mara 2 kwa siku na wanaume tofauti...iweje akwambie mmoja tu...
 
Mkuu hata usiangaike we fanya hivi zidisha caring tu mwanamke ashaamua we just muunge mkono tu ila kuwa na tahadhari haya mambo ni mazito ukienda kichwa kichwa
 
Back
Top Bottom