Huyu hapa Rais 2025 ili tuvuke salama

Huyu hapa Rais 2025 ili tuvuke salama

MSHINO

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,069
Reaction score
713
Nikuu kutoka maktaba: Dar es Salaam. Baadhi ya wananchi wamekuwa na maoni tofauti kuhusu namna sakata la wizi wa fedha kwenye akaunti ya Escrow linavyoshughulikiwa, huku wengine wakisema umefika wakati sasa nchi iongozwe na rais dikteta.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, walisema kuwa uamuzi wa Naibu Spika,
Job Ndugai kuwaomba wabunge kukishauri kiti chake juu ya hatua ya kuwasilishwa na kujadiliwa kwa ripoti ya uchunguzi wa fedha za Escrow, umeonyesha Bunge linataka ukweli ujulikane.

Mratibu wa Umoja wa Wanawake Wanasiasa Tanzania (ULINGO), Dk Ave Maria Semakafu alisema baadhi ya watu wanataka kupotosha ukweli kwa kuwataja viongozi wasiohusika hawahusiki moja kwa moja na ufisadi wa fedha hizo badala ya kuwanyooshea kidole majaji waliotajwa kupewa mgawo huo.

Akizungumzia suala la mahakama kuzuia jambo hilo kujadiliwa bungeni, alisema kinachofanyika ni sawa na kumpa nyani kesi ya ngedere huku ukijua kabisa haki haitotendeka.

“Hata waandishi wa habari wanakosea mahali pa kulenga, majaji watatu ndio wametajwa kupata mgawo (anawataja), suala hapa Jaji Kiongozi atoe taarifa kuhusiana na jambo hilo,” alisema Semakafu.

Alisema kutokana na kujirudiarudia kwa matukio ya ufisadi nchini, taifa limepoteza mwelekeo hivyolinahitaji kiongozi dikteta atakayeweza kuwashughulikia wahalifu bila huruma.

“Nchi haijulikani inakwenda au inarudi. Dawa ni kupata kiongozi dikteta, nchi hii haihitaji mtu mwenye makundi, tumefika hapa kwa sababu ya urafiki,” alisema Semakafu.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa George Shumbusho alisema kinachoonekana sasa ni matokeo ya viongozi kutokuwa na utamaduni wa kuchukua hatua
kali watu wanapofanya makosa, ikiwamo kufilisi mali zao. Profesa huyo alisema kwa hali ilipofikia nchi inahitaji kupata kiongozi dikteta ambaye atakuwa tayari kutawala kwa muda mfupi ili arudishe nidhamu iliyopotea. “Tunahitaji dikteta atakayesema nitakaa kwa muda mfupi, asafishe uozo, kisha aondoke, Haiwezekani tuendelee kushuhudia nchi ikizidi kufilisika,” alisema Profesa Shumbusho.

Mbunge wa Mgogoni, Kombo Khamis Kombo (CUF), alisema matukio ya ufisadi yameongezeka nchini kwa sababu kila kiongozi anayetarajiwa kuchukua hatua analalamika. kuwa watendaji wake wanamwangusha. “Viongozi wanapiga danadana, wana watu ambao hawawezi kuwakosoa…, tulipofikia tunahitaji kiongozi mwenye maadili,” alisema Kombo.

Mkuu wa Kitivo Msaidizi (Taaluma), Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam, Danford Kitwana alisema kilichotokea bungeni juzi kinaashiria Serikali.

kujaribu kulizima suala la Escrow ili lisijadiliwe kwa kuwa wanafahamu linaweza kuwang’oa baadhi ya viongozi madarakani. Hata hivyo, alisema kutokana na kauli za wabunge wengi waliotoa mapendekezo yao kutaka jambo hili lijadiliwe na ukweli kufahamika, Serikali itakuwa na nafasi ndogo ya kukwepa kutekelezwa kwa maoni ya wabunge walio wengi.

Aliongeza: “Tatizo la Tanzania ni ukosefu wa maadili na uchungu wa mali ya umma, tutaendelea tu kusikia kesi kama hizi kwani bado kuna mambo mengi yaliyofanywa bado hayajafichuliwa.”
 
Tundu lissu aliwataja wote kwenye Bunge la makinda.

Hii nchi inalana
 
Kuyawazia ya 2025 wakati hata bado ya 2020 hadi 2025 hatujayamaliza au kuyashuhudia ni Kupotoka mno Kifikra kwa Wanaojiita Wasomi nchini.
 
Mnatamani miaka iende haraka jamaa atoke ha ha ha tuna safari ndefu mno.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, walisema kuwa uamuzi wa Naibu Spika,
Job Ndugai
Mkuu, umekopi na kupaste habari ya zamani nini? Hivi Job Ndugai ni naibu spika?

Kwa taarifa yako, kukopi na kupaste habari iliyoandikwa na mtu mwingine bila kuacknowledge ni kosa, inaitwa plagiarism.

Weka jina la mahali ulikotoa habari yako. Kusema 'nukuu kutoka maktaba' haitoshi!
 
Back
Top Bottom