Huyu hapa NYOKA

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,440
Reaction score
38,437
I like this msg.

Bwana mmoja alimuona nyoka akiungua na moto kiasi afe, akaamua aokoe maisha yake kwa kumtoa. Alipofanya hivyo aling'atwa na yule nyoka na kumuachia maumivu makali yaliyosababisha amuachie na hatimaye yule nyoka akaangukia tena ktk moto. HATA hivyo yule bwana aliamua kumuokoa tena yule nyoka ila safari hii akichukua tahadhari asing'atwe tena.

Mtu mmoja shuhuda wa lile tukio akamuuliza "ya NINI ujisumbue kuokoa maisha ya huyo nyoka aliyehatarisha maisha yako kwa kukung'ata?"

Yule bwana akajibu, kung'ata nyoka ni asili yake, nami kusaidia ni asili yangu

Wapo watu utakaojitoa kwao na kuwasaidia kuwatoa katika hatari ila mwisho wa siku watakung'ata na kukukejeli. Hawana shukran.

Inafika mahali na wewe unataka kuwa kama wao, KUMBUKA,

Wapo ambao hiyo ndio sifa yao...Wewe fanya moyo wako ulivyo.
Usilipe baya kwa baya na wala usipoteze moyo mwema ulionao, ila jifunze kuchukua tahadhari.

Kazi ya Control C na Control V
 
Jamani,,,, Basi atatuumiza sana maana anangata kotekote
 
Naju
Najua unamaanisha mini, tens najua unamsema nani.
Mbele kwa mbele lakini.
 
Ime kaa poa tena sana [emoji871]
 
Nilichogundua ukiwa na roho nzuri (walio wengi) huwezi kubalika hata utendewe vipi? Ni rahisi kwa mwenye roho mbaya kubadilika kuwa mwema kuliko mwenye roho nzuri kubadilika kuwa mbaya.
kuna cha kujifunza hapa!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…