Huyu Ernest Massawe ni nani?


hili ndiyo jibu.
 
Huyu jamaa ni miongoni mwa watu wenye maeneo makubwa sana na mengi ya uchimbaji wa madini hapa nchini.

Karibu nusu ya vitalu vya uchimbaji dhahabu mkoani Geita na hasa eneo la Lwamgasa,Nyarugusu,na Nyaruyeye.
 
Ernest Massawe ni msomi,aligraduate university of East Africa (Nairobi) kitaaambo sana,then akapata ACCA,akaanzisha kampuni yake ya auditing,Massawe Ernest auditing firm ndio bwana young akaja wakaunganisha nguvu mpaka kampuni imekuwa kubwa na yeye ndio chairman kwa africa mashariki,anamiliki makampuni mengi na ameihusisha familia yake kwa ukaribusana sababu ni wasomi wakubwa pia,sasa ni chairman wa swala!
 
Mkuu huyu jamaa nasikia hata kumwona ni shida anamzigo wa kufa

Mkuu kumwona sio shida, sisi mbona tunapiga nae mvinyo huku bahari beach. Ni mzee poa sana, ana makazi yake ras kilomoni, beach residence. Ni jirani yangu na watoto wake andrew (Dru ) na Justine ni washkaji sana tu. Hii family iko humble sana.
 
Duu huyo kweli katumia vyema elimu yake,kuna watu wana viCpa vyao huko serikalini wanajiona miungu watu
 
Duu huyo kweli katumia vyema elimu yake,kuna watu wana viCpa vyao huko serikalini wanajiona miungu watu

Wengi wanajisahau mkuu. Kuajiriwa mpaka unastaafu bila kuanzisha kitu chako ni ulimbukeni wa hali ya juu. Wengi wanaishia kujenga majumba makubwa kwa mkopo na magari makubwa, wakistaafu wanakuwa chali kama kifo cha mende
 

Mkuu, penye mikolezo umekosea. Hiyo kampuni inaitwa Ernst (sio Ernest) & Young (kwa sasa EY tu). Ni kampuni ya zamani sana ya Marekani/Uingereza. Huyo Massawe alifanya kazi sana huko ujanani kwake. Nadhani bado ni partner ila si mwanzilishi wa hiyo EY.
 

Hata mimi nilishangaa kampuni ilikuwepo tangu mwaka 1839 huyu jamaa kafanya nao merger lini?
 

Ni jirani yangu pale Rombo, nakumbuka mashine za kusaga mazao pale kwake, ni pete na kidole na Bazili Mramba,.. Ana skendo nyingiii tuu...
 

Jadilini the so called wawekezaji wa nje ambao wanapora mali zetu au wamegeuza tz shamba la bibi.
 

Kweli unajiona umeandika jambo la maana? Maana hayo yote uloponda yanakuhusu ndio unayajua au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…