Huyu bibie simuelewi, au ndio maringo au vipi?

fundi bishoo

JF-Expert Member
Jun 26, 2018
12,956
22,650
Habari wazee wakubwa shikamooni pia poleni na majukumu,

Miezi kama minne iliyopita hapa mtaani kwetu kuna demu mmoja mzuri tu alimtumaga mtoto aje kwangu anipe karatasi imeandikwa namba yake ila yule dogo alivokuja kunipa ile karatsi hakujieleza vile halafu alikuwa kama anatania hivi mimi nikamuona dogo anazingua nikamfukuza sasa baada kama ya mwezi hivi nikakutana na yule dogo nikamuuliza ile siku ulikuwa umetumwa au unanizngua?

Dogo akanambia kuwa alitumwa kweli na huyo demu basi daah roho ikaniuma halafu yule msichana huwa anakuja na kuondoka tu hapa mtaani,huwa anakuja kuwatembelea ndugu zake.

Basi ikapita kama miezi minne nikaja kumuona yule demu ila mazingira yakawa hayaruhusu lkn siku moja kama Mungu aliniona demu nilimuona nikawa nalazimisha namba yake lakini alikuwa ananikazia. Nimelazimisha sana baadae akakubali kunipa ikawa nkimtumia meseji tunachati kdg halafu ananipotezea (kumbuka tukio la nyuma sijawahi kumuambia hapo)

Basi nikaona labda kama alinimind kutokana na kipindi cha nyuma nlivyomfanyia basi nikamtumia meseji ya kumuomba msamaha kuhusu kipindi cha nyuma demu anjifanya hajui chochote halafu kaniambia hajawahi kufanya upuuzi kama huo.

Basi mimi nikajaribu kubadilisha stori pale lkn wapi hakunijibu meseji zangu wala nini na mimi nikapotezea.

Toka ile siku mpaka leo sijamtafuta wala nini ila natamani kumcheki lakini ananikatisha tamaa.

Ndugu zanguni nipeni mawazo yenu kuhusu huyu bibie maana nampenda pia.
 
Dah...ingekuwa ya kiingereza ningetiririka...ila kiswahili hata sijui nianzie wapi
emoji2960.png
 
Back
Top Bottom