Huyu anaweza kwenda ualimu?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,089
114,626
Ana Div 4 ya 28....Maths,Bios,Civics,B/Keeping,History,Geog,Kisw,English yote D,Commerce F.Maombi ya vyuo vya serikali yapoje?
 
duuuhhh Yani ualimu ndo kimbilio la walofeli,,,,sijui watawafundishaje wanetu
 
Kama ni kijana ambaye havai mlegezo anaweza akaenda.... Maana siku hizi kuna uhaba wa vijana wanaojua kuvaa suruali vizuri kwenye kiuno. Hakuna uhaba wa ufaulu...
 
Ana Div 4 ya 28....Maths,Bios,Civics,B/Keeping,History,Geog,Kisw,English yote D,Commerce F.Maombi ya vyuo vya serikali yapoje?
Acha hofu ukisikiliza ya watu utashindwa kufanya yako!! Ualimu kwa sasa wanachukua 1-3 kwa ngaz ya diploma! Chakufanya unaweza kusubiri vyuo vya utumishi wa umma na vingine ving tuu anaweza kusoma!! Asiogope kila kitu kinawezekana!! Pia asiache kuangalia NACTE wakitoa matangazo yao na vigezo mbalimbali wanavyohitaji huenda akabahatika kupata koz nzuri ya kusoma!!

Kwa aliekwenda shule na kuelewa anajua nn maana ya kufeli na kufaulu hatujui inaweza ikawa ilikuwa ni haki yake kupata hivyo au ni external factor zilizomfanya apate hayo matokeo!! Wangu ushauri tuu!

Ahsante
 
Kwa matokeo yako unaweza kuwa na machaguo kadhaa lakini Mimi nashauri kama unaouwezo na ungependa kuwa mwalimu.
1. Unaweza kurudia mitihani yako ya kidato cha nne, kama unaweza na unafikiri unaweza Fanya hivyo.
2. Soma kozi ya mwaka mmoja katika fani yoyote ufaulu kisha ujiunge na chuo kikuu huria kwaajili ya foundation course mwaka mmoja inahitaji uwe na pass 4 (D NNE) na umesoma kozi nyingine isiopungua mwaka mmoja na kufaulu, ukifaulu foundation course unaweza kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza.
Usikate tamaa uko vizuri
 
Back
Top Bottom