Huyo jamaa hapo chini inasemekana amekutwa akiwa an mke wa mtu

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Huyo jamaa hapo chini inasemekana amekutwa akiwa an mke wa mtu hivyo mwenye mke akaamua kumfanyizia kama inavyoonekana kwenye picha!

Sasa swali langu kwanini ufanye hivi kama ukimfumania mke wako? Kwangu mimi ni ujinga unaochangiwa na IQ ndogo kwa upande wa Mwanaume yaani uwezo mdogo wa kufikiri, kwa maana huyo Mwanaume ana kosa gani? Kwani kambaka mkeo? Mke wako amekubali mwenyewe kulala na Mwanaume mwingine hivyo ulipaswa udili na Mke wako na siyo Mwanaume aliyelala na Mke wako!

Raisi Magufuli ametangaza kwamba sasa ni wakati wa TanZania ya Viwanda yaani ku-indutrialize TanZania sasa kwa watu wenye reasoning kama hawa wetu ni ngumu kuona jinsi gani tunaweza kweli kuindustrilaize nchi yetu, kwa maana tunahitaji uwezo mkubwa wa kufikiri wa watu wetu na siyo kufikri kama kijana wa miaka 13 kwani ni kwanza tunajitaji kubadilika (mindset) !

Hao ndiyo wanapaswa kuwa watafiti na wabunifu wetu na kupatent ubunifu wao kwa ajili ya Viwanda vyetu!
123img.PNG

Hii ndiyo aina ya watu ambao wanapaswa kukaa nyuma ya Computer na kutengeneza softwares kwa ajili ya Viwanda vyetu!
IMG20150510WA0009.JPG
 
Jamii iliyoendelea ama inayotaka kuendelea kufikia huku unaposema kwenye industrialization lazima ianze na watu wenye maadili....Hakuna cha kusema ukikuta mtu anatembea na mke wako utadeal na mke wako na jamaa alikupigia mama utamwacha hii haipo...Imagine jamaa ni rafiki ako kabisa then anamshawishi mama kupitia udhaifu wa mama jamaa akila mzigo...real we mwanaume ambaye ni rafiki angu na ukala mama sintokuacha maana umenidharau na labda uliamini sintokuweza...Kwanza ntakufanyia kitu ili iwe fundisho kwako na mama nae kama kuna adhabu yake itafuata ila na wewe hutobaki salama....
 
Lkn swali linakuja kwa kumdhuru huyo Mwanaume umetatua tatizo? Hilo ndiyo swali la msingi hapa, yaani kiini cha sababu ya Mke wako au niseme Mke wa mtu kutembea na Mwanaume mwingine nini?
Haya tuseme umemfanyizia huyo jamaa halafu kwa bahati mbaya akafariki unafikiri Mahakama itakuelewa? Wewe si utapewa kesi ya mauaji na hauoni kwamba hapo itakuwa ndiyo maisha yako yameharibika forever? Au kesho kutwa tena mke wako akatembea na mwingine bila ya wewe kujua utafanyaje? Au hata ukijua utamfanyizia pia? na je yule unayetaka kumfanyizia na yeye akikutaimu akakuvunja mkono au kiungo chochote cha mwili halafu itakuwaje?
 
ww hivyo huyo mke umetftiwa au umemtqfta mwenyewe kwann usife kwaajili ya chako na we utataka maendeleo gani wakt hujui jinsi ya kudai haki yako na kifup binafs hatq kulipuka naye mie nalipuka tu sintojali kuvunjwa kiungo
 
Anayejihusisha na mwanaume aliyezini na mke wake hana akili kabisa. Kwani mkeo taahira anayekubali kila anayemtongoza? Ukioa malaya usigombane na wanaume kwa sababu wengi watakaomlala hautawaona, piga talaka tupa kule
 
Huyu mume tatizo ana kibamia, ingelikuwa ana mtarimbo wala yasingelimtokea yote hayo. Una rambo nna muwa
 
Mkuu wewe piga tarumbeta weee, ila nakuambia tu weka akilini hii.MKE YA MUTU NI MWIKO.Ogopa.

Toka nimezaliwa sijawahi kuona mtu kamfumania mwanaume na mkewe, akamfanya chochote atakachojiskia hadharani mwanaume yule halafu jamii ikamlaumu.kwanini????? Mke anauma kuliko msiba.

Nashangaa digital mnataka kuhalarisha huu ubazazi wa kubeba wake za watu kujidai hamna makosa.hii haipo.

Utabakwa tu, ukikutwa tigo itasambaratishwa maana imeandikwa na wenye wake zao kwamba kila mtu aoe wa kwake hata kumi akitaka.
 
Inasikitisha watanzania kuhangaikia vijimambo vyepesi vyepesi kama ugoni! Mwanamke aliyeshikwa ugoni ni mtu mwenye akili timamu na ana uwezo wa kuamua kuvunja mkataba wa ndoa wakati wowote, suluhisho ni kumwacha na kuchukua mwingine lakini hilo la kumvua mtu nguo, kumpiga na kumdhalilisha mwanaume ambaye pengine hata alikuwa hajui kama yule mama ni mke wa mtu ni wazimu unaoweza kukuangamiza.
Wahusika katika picha hiyo wanaweza kuwajibishwa kisheria kama aliyedhalilishwa ataitafuta haki kisheria maana kama ni kosa Mahakama zipo na mbaya wakimuua watakabiliwa na kesi ya mauaji wanyee ndoo miaka hadi miaka wakimwacha mwanamke anapeta na wengine. Kwa mtaji huu maendeleo ya kweli Tanzania ni ndoto maana mawazo ya Watanzania wengi tumeyaelekeza kwenye zipu! Ovyo!!
 
Kwani nchi zenye viwanda hawafanyagi Watusi??
Wanafanya matusi sana ila hawaendekezi ujinga kama huu wa kuabudu mwili wa Binadamu! Nimekaa sehemu kadhaa kwa muda mrefu tu kwa wenzetu wa nchi za viwanda
wanajali zaidi kazi na fedha kuliko sisi.
Kwa asilimia kubwa ni waaminifu kwa wenzao wao na mmoja anapoonekana kuchepuka sijaona wala kusikia ushamba wa namna hii wa eti mtu aende na wapiga picha amtembeze mwanamke au mwanaume hadharani, sana sana ni kuachana kistaarabu na kila mtu kuendelea na maisha yake. Kwa wenzetu waliendelea (nchi za viwanda) muda ndiyo kitu muhimu zaidi kuliko kuabudu ngono kama tulivyo, kuendekeza ngono na starehe na kusahau kabisa utafutaji!
 
Jamii iliyoendelea ama inayotaka kuendelea kufikia huku unaposema kwenye industrialization lazima ianze na watu wenye maadili....Hakuna cha kusema ukikuta mtu anatembea na mke wako utadeal na mke wako na jamaa alikupigia mama utamwacha hii haipo...Imagine jamaa ni rafiki ako kabisa then anamshawishi mama kupitia udhaifu wa mama jamaa akila mzigo...real we mwanaume ambaye ni rafiki angu na ukala mama sintokuacha maana umenidharau na labda uliamini sintokuweza...Kwanza ntakufanyia kitu ili iwe fundisho kwako na mama nae kama kuna adhabu yake itafuata ila na wewe hutobaki salama....
Fikiria nje ya box .Mara nyingi sio rafiki yako.mkeo katongozwa mtaa Wa pili au mkoa mwingine na akajitambulisha kuwa hana bwana .huyo mtu ukimfumania nae utamfanyaje nae !!??.ukweli unabaki pale pale wewe dili na mkeo mwanaume utakae mfumania nae msalimie na mwache aende zake .dili na kahaba wako uliye mfuga .
 
Huyo jamaa hapo chini inasemekana amekutwa akiwa an mke wa mtu hivyo mwenye mke akaamua kumfanyizia kama inavyoonekana kwenye picha!

Sasa swali langu kwanini ufanye hivi kama ukimfumania mke wako? Kwangu mimi ni ujinga unaochangiwa na IQ ndogo kwa upande wa Mwanaume yaani uwezo mdogo wa kufikiri, kwa maana huyo Mwanaume ana kosa gani? Kwani kambaka mkeo? Mke wako amekubali mwenyewe kulala na Mwanaume mwingine hivyo ulipaswa udili na Mke wako na siyo Mwanaume aliyelala na Mke wako!

Raisi Magufuli ametangaza kwamba sasa ni wakati wa TanZania ya Viwanda yaani ku-indutrialize TanZania sasa kwa watu wenye reasoning kama hawa wetu ni ngumu kuona jinsi gani tunaweza kweli kuindustrilaize nchi yetu, kwa maana tunahitaji uwezo mkubwa wa kufikiri wa watu wetu na siyo kufikri kama kijana wa miaka 13 kwani ni kwanza tunajitaji kubadilika (mindset) !

Hao ndiyo wanapaswa kuwa watafiti na wabunifu wetu na kupatent ubunifu wao kwa ajili ya Viwanda vyetu!
123img.PNG

Hii ndiyo aina ya watu ambao wanapaswa kukaa nyuma ya Computer na kutengeneza softwares kwa ajili ya Viwanda vyetu!
IMG20150510WA0009.JPG
HAWA jamaa ndugu nini mbona wamefanana sana !!??
 
Dawa ya hawa wanaotembea Na wake za watu ni kuwauwa tu. Na hii haina uhusiano wowote Na mapinduzi ya viwanda.
 
Dawa ya hawa wanaotembea Na wake za watu ni kuwauwa tu. Na hii haina uhusiano wowote Na mapinduzi ya viwanda.

Tuseme umefanikiwa kumuua halafu ni nini kitafuata? Unafikiri Vyombo vya Dola vitakuacha na kukuelewa kwamba umemua kwa sababu alitmebea na mke wako? Watakuchukuwa na utafunguliwa kesi ya mauaji na utafungwa maisha, sasa ndiyo utakuwa umefaidika nini? Vipi Watoto na familia yako huku nyuma? Vipi kuhusu Mali na kazi yako? Inabidi ufikirie mbali zaidi na usikubali binadamu mmoja yaani Mwanamke ndiyo aamue hatima ya maisha ya yako, kama mke wako anatembea na Wanaume wengine ina maana Mke wako ndiyo ana matatizo na wewe na siyo yule anayetembea naye, na isitoshe yeye ni Mke wako lkn siyo mali yako!
 
Hata mimi sioni logic! Huku ni kuivunjia heshima maana halisi ya JF . Is this really great thinking !
Tatizo la Ndugu Barbarosa yeye kila kitu anakiangalia kwa jicho la ki Siasa.
Nna uhakika kabisa alitaka kusema hao jamaa waliofumaniana ni wana UKAWA / CHADEMA.
 
Back
Top Bottom