Huwezi kuwasaidia wengine bila kujisaidia wewe kwanza

Huwezi kuwasaidia wengine bila kujisaidia wewe kwanza

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,204
Leo nitie neno kidogo wakuu ni kama kukumbushana tu kwa sisi vijana watafutaji,
"Huwezi kuwasaidia wengine bila kujisaidia wewe kwanza"

Kijana wakati wako wa kutafuta maisha tafuta ukiwa na nia moja tu ya kujisaidia wewe kama wewe ,usije kutafuta maisha ukiwa na list ya watu wengi wa kuwasaidia hapo uwezo wa kuyawini maisha unakuwa ni mdogo sana,

Ukishatafuta na kupata ndio huwe na mawazo ya kutoa msaada tena toa msaada kwa kile ambacho hakitaadhiri uchumi wako,

Ndugu na jamaa watakupenda tu pale ukiwa na kitu,utawapa misaada na kila kitu lakini siku ya Anguko lako hakuna kitu hutaacha ona ,nyodo,masimango plus kutengwa nafikiri unaweza kufa kwa depression kila utakapokumbuka ya nyuma,

Siku zote waza kuhusu future yako acha kuwaza wengine na ndio maana kuna maandiko yanasema "Kila mtu atabeba msalaba wake"
 
Tanzania asilimia 70-60 ni breadwinners/tegemezi,30% ndio watafutaji
 
Back
Top Bottom