Asalam Aleykum,
Bwana Yesu Asifiwe,
Tumsifu Yesu Kristu,
Mwanakondoo Ameshinda,
Bwana ni Mwema.
Ama baada ya salamu hizo, naomba niende kwenye mada tajwa hapo juu.
Baada ya uchaguzi wa CHADEMA kukamilika, wale waona mbali lazima walijua kile ambacho kitaipata CCM.
Hawa jamaa watatu ni hatari sana kwa CCM.
Kwa sasa tunaweza tusikubaliane, lakini kadri siku zinavyoenda, tutakuja kuelewana siku moja.
Katika historia ya Tanzania, hatujawahi kupata upinzani kama huu upinzani uliopatikana.
Itoshe tu kusema, mwaka huu endapo uchaguzi utafanyika kwa Uhuru na Haki kabisa, Upinzani unachukua madaraka asubuhi na mapema.
Mgombea Urais kupitia chama tawala bahati nzuri tunamfahamu vizuri pamoja na uwezo wake wa kujenga hoja.
Na kama ilivyo mara zote, wafuasi hawawezi kumzidi kiongozi wao namna ya kujenga hoja. Tumeona akina Makalla juzi na hoja zao kwamba upinzani wanajipanga kununua virusi sijui vya mpox na ebola, wote tumekuwa tunamsikia wasira toka ateuliwe umakamu, uwezo wake wa kujenga hoja wa zamani na sasa ni vitu viwili tofauti kabisa. Wasira wa zamani alikuwa vizuri sana kichwani kulinganisha na huyu wa sasa. Mbali na uzee, bado ile asili ya kwamba sikio haliwezi kuzidi kichwa inabaki pale pale na bahati mbaya huwezi kwenda kinyume na asili! Wafuasi mara zote wanakuwa kama kiongozi wao.
Sasa tukija upande wa upinzani, Tundu Antipas Lissu, John Heche na Godbless Lema, wote hawa wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa wa kujenga hoja.
Wote wako vizuri sana kichwani na wana hari kubwa sana. Kiufupi ni wamejipanga vilivyo kuing'oa CCM madarakani wakati huu na siyo 2030!
Wakati mwingine nafikiria TumainiEl wakati ameleta kisa cha Simba Bob aliyeshindwa na Simba madume watatu, basi huenda Bob alikuwa ni BWANA HURU na hawa watatu walikuwa LAT, HJ na LG. Na kama sitakuwa mbali na ukweli, basi mama wa watu kazi anayo, labda vyombo visimame kidedea kuingilia kati maana hawa Simba ni hatari sana na inavyoonekana hawaogopi chochote na hakuna cha kuwazuia.
Kwanza mvuto wao kwa jamii unaongezeka kila uchao, fuatilia hata sehemu wanazoenda namna wanavyokusanya kijiji.
Pili hali ya uchumi kwa wananchi wengi ni ngumu sana kutokana na mfumo mbovu wa uongozi uliopo.
Tatu vijana wengi hawana ajira na badala ya kupewa matumaini na viongozi badala yake wanapewa kauli za kejeli za kwamba warudi VETA wakapate ujuzi wakati ujuzi wenyewe walishaupata vyuoni na wengine kama haitoshi wamefanya hadi "internship" sehemu mbalimbali.
Nne, mvuto kwa viongozi wengi waliopo ni wa kutafuta kwa tochi, sema mikutano yao mingi huwa inajazwa na wanafunzi na watu wa kubebwa na malori pamoja na mabasi. Na nasikia tayari chama kimeshanunua mabasi mengi kwa ajili ya hiyo kazi!
Tano, uchaguzi wa CHADEMA ni kama ulihusisha Watanzania wote waliopo ndani na nje ya nchi, hivyo hata viongozi waliopatikana ni kana kwambq wamechaguliwa na Watanzania wote kwa maana wote tulihusika.
Sita, wanaharakati wengi wako upande wa CHADEMA, ukianza na Rais wa TLS Mh. Wakili Msomi Mwabukusi, Mama Anna Nkya, mama Anna Tibaijuka n.k.
Saba, jamii imechoshwa na unyanyasaji dhidi ya wananchi wakiwamo wamasai waliolazimishwa kuondoka Ngorongoro ili wamwachie Mwarabu.
Nane, uuzwaji na umilikishaji wa Raslimali mbalimbali za Taifa kwa wageni ilhali kama nchi tulitumia gharama kubwa kuzitengeneza mfano Bandari ya DSM kupewa DPW, ile ya Bagamoyo nasikia wamepewa Waarabu wa Saudia n.k
Tisa, mparanganyiko utakaotokea ndani ya chama tawala. Historia inaonesha kila wakati wa uchaguzi lazima kuna wale ambao huja kujiunga na upinzani toka chama tawala ambapo wengine huja na "mafuriko" kama ilivyokuwa kwa marehemu Mrema 1995, na marehemu Lowassa 2015. Hapo bado wale watakaokosa nafasi za ubunge ambao watakuja upinzani ili wapate nafasi n.k
Mwisho, hawa jamaa ni kama wameandaliwa kwa wakati huu. Kulingana na historia ya ulimwengu, mabadiliko ndo suala pekee lisilobadilia, yaani; "Only change is constant".
Nimalizie kwa kukiri kwamba pamoja na kwamba mimi siyo mwanachama wa CHADEMA, lakini kwa huu upepo, nimeamua kuwaunga mkono na tayari nimeanza kuwachangia kwenye kampeni yao ya Tone Tone. Na mimi nimeweka tone langu ambalo likiungana na matone ya wengine wenye mapenzi mema na ukombozi wa Taifa hili, basi mafuriko lazima yatokee.
Kama taifa, tumechoka kuongozwa na tusiowachagua maana hata katika kutoa huduma mara nyingi huonekana kama wameshiba sana na wengi wao wanakuwa na dharau kwa sababu wanajua fika kwamba wewe mwananchi hukuwaweka kwenye hizo nafasi wanazozishikilia. Hivyo tuwaunge mkono hawa ndugu zetu watatu, Tundu Lissu, John Heche na Godbless Lema ili tupate mabadiliko kwanza ya Katiba, halafu ya Tume ya Uchaguzi. Hii huenda ikatusaidia angalau kuongozwa na tuliowachagua aidha sisi wenyewe au na wale tuliowatuma kuifanya hiyo kazi.
Tunataka Rais apunguziwe majukumu na madaraka maana aliyonayo ni makubwa sana.
Ahsanteni sana.