Huu usafi wa kila mwisho wa wiki sasa ni kero

Malcolm X5

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
1,637
2,748
Order ya kwanza iliyotoka kwaRais JPM ilikuwa ni Jumamosi ya mwisho wa mwezi,sasa naona kuna nyingine,nimeamshwa Leo asubuhi sana kufanya usafi nikidhani utani,natoka naelekea kibaruani njiani maduka yamefungwa,najiuliza eenh kumbe ni wilaya nzima au?,ole wako wakute duka wazi.

Wanadhani watu wote ni wa serikali,wa kupumzika Jumamosi,mtu asifanye biashara mpaka saa NNE kweli?,na biashara ilivyo ngumu hivi.
 
Jamani kuna watu kama mimi nakula kwa kupekuwa kama kuku sasa ukinifanya niwe na jukumu lingine itabidi tu wape bank account wawe wanatulipa na sisi kila mwisho wa mwezi
 
Sasa bado tuko boarding hapa,kwani wote unadhani tumelelewa kwa kususwa na wazazi wao,mtu una miaka miwili tu unaanza boarding,ndio akili zenyewe
Sasa kama hauko boarding kwa nini wakubwa wazima mnaambiwa kusimamiwa kufanya usafi kwa faida yenu wenyewe.

Asiyefunzwa na mama yake hufunzwa na ulimwengu, vumilia ndg yangu wakati ulimwengu unakufunza, fanya usafi please onnyesha ushirikiano.
 
Order ya kwanza iliyotoka kwaRais JPM ilikuwa ni Jumamosi ya mwisho wa mwezi,sasa naona kuna nyingine,nimeamshwa Leo asubuhi sana kufanya usafi nikidhani utani,natoka naelekea kibaruani njiani maduka yamefungwa,najiuliza eenh kumbe ni wilaya nzima au?,ole wako wakute duka wazi.

Wanadhani watu wote ni wa serikali,wa kupumzika Jumamosi,mtu asifanye biashara mpaka saa NNE kweli?,na biashara ilivyo ngumu hivi.
Cha ajabu wanafanya usafi barabarani tu makwao ndani hawafanyi
 
Sasa kama hauko boarding kwa nini wakubwa wazima mnaambiwa kusimamiwa kufanya usafi kwa faida yenu wenyewe.

Asiyefunzwa na mama yake hufunzwa na ulimwengu, vumilia ndg yangu wakati ulimwengu unakufunza, fanya usafi please onnyesha ushirikiano.
Eheheh mnachojua tu ni kufua socks,sasa ulimwengu unafundisha nn hapo?,nyumbani si pachafu,usumbufu tu,manual,imagine unaanza kindergarten mpaka university uko boarding,alafu unaingia serikalini,sijui hata kama maisha ya mtaani mnayajua nyinyi kwa kuongea tu kwenye maforums humu,silly,nchi inaongozwa kwa mihemko,eti issue ni boarding eheheh
 
Haujielewi kama unapinga suala la usafi, issue ya usafi ni mhimu sana especially mazingira ya biashara na Maeneo ya makazi, watanzania wengi hatuna utamaduni wa kufanya usafi wa hiari, acha tushurutishwe.

Maeneo mengi ni machafu kupindukia tufanye usafi na serikali ifanye yake kupitia manispaa washafishe Maeneo ya mhimu.
 
Usafi ni muhimu sana Wilaya ya Ngara mkoa wa kagera Kila alhamisi kuanzia asubui -saa nne n usafi mwanzo mwisho na ile wameiga rwanda imetokea Ngara kua wilaya safi kabisa ila Kwa Dsm labda wamwagw wajeda na fimbo mana watu wako resi mbaya...
 
Hivi kwa nini kila mtu asifagie nyumbani kwake?...Kuliko wote twende tukarundikane sehemu eti tunafanya usafi...Hii nami imenikuta leo asubuhi wamekuja kugonga eti tukafanye usafi...Nimewaambia acheni Ujinga naenda shambani...Sehemu yangu nimeshafagia.

MAMA TERESA ALIWAHI SEMA KILA MTU AKIFAGIA NYUMBANI KWAKE BASI DUNIA NZIMA ITAKUWA SAFI.
 
Back
Top Bottom