Huu si wakati wa kutaharuki mh Rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu si wakati wa kutaharuki mh Rais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by everybody, Mar 4, 2011.

 1. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama huu ni wakati wa Rais Kikwete kutaharuki na kuanza kuongelea maswala ya machafuko kama alivyokuwa akisisitiza kwenye hotuba yake. Nadhani suluhisho hapa ni kwa viongozi wote wakuu wa vyama ikiwemo CCM kukaa pamoja na kujadiliana wakati wa matatizo ya dharura. Nadhani kama wenyeviti na makatibu wakuu wa vyama (CCM na wapinzani) wakikutana wanaweza wakatoka na mawazo yenye kujenga. Tuache siasa wakati wa matatizo serious kama ukosefu wa umeme na chakula.
  Pia sidhani kama viongozi wa CCM akiwemo Rais wanatakiwa kuongelea maswala ya machafuko na umwagaji damu. Hii inasabisha hayo mawazo kuingia akilini mwa watu. Sidhani kama kuna mtu anamawazo ya kumwaga damu. Wanachofanya CHADEMA ni siasa tu na sidhani kama kuna haja ya CCM kuchanganyikiwa kwa sababu utendaji wao kama hauwaridhishi wanachi wataondolewa tu ikifika 2015. Wao kama kweli wanadhamira ya kuondoa matatizo ya wananchi wawashirikishe pia viongozi wa upinzani hasa wakati wa dharura na kupata mawazo. Viongozi wakuu wa vyama waache viburi vyao, wakae pamoja. Hakuna aliyemjuaji kuliko mwenzie na hakuna mtu anayeweza kupredict future with certainty hasa ikiwa unategemea mvua kwa kiasi kikubwa katika maisha yako ikiwemo mvua kwenye umeme, mvua kwenye chakula, etc....
   
Loading...