Tajiri la Bitcoin
JF-Expert Member
- Apr 9, 2017
- 1,148
- 711
Wanabodi,
Wasalaam,
Huko Mkoani Shinyanga mwenyekiti wa Wilaya wa Chama cha mapinduzi (CCM )wilaya ya Shinyanga Abouh Gulamu akiwa na timu yake amewafuata baadhi ya wenyeviti wa mitaa wa CHADEMA na kuwataka wahamie CCM kwa lazima na wasipofanya hivyo yatawakuta yaliyomkuta mbunge wa Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nassar.
Wenyeviti waliofatwa ni pamoja Mh. Kerenge Nyakaganda ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Banduka na Mh. Ayoub Daniel Ayoub mwenyekiti wa mtaa wa Mapinduzi wote wanatoka kata ya Ndala. Pia wajumbe wa serikali za mitaa ambao ni Robert Chacha, Haji Kija, Deo Masanja pamoja na Perepetua James. Viongozi hawa wamepewa ahadi nyingi na kama hawataondoka kwa hiari kuna vitisho pia. Hata hivyo viongozi hao wamegoma kusaliti maamuzi ya wananchi waliowachagua na kwamba wataendelea kuwatumikia. Wamesema dhambi ya usaliti kwa wananchi ina hukumu sawa na dhambi ya Yuda Iskarioti hivyo watabaki kuwatumikia wananchi wao wakiwa CHADEMA.
CCM MMEKATALIWA NA UMMA ACHENI VURUGU MWONDOKE KWA AMANI 2020.