Huu ni ujumbe kwa dada zangu

gasgas

JF-Expert Member
Jan 25, 2015
1,090
978
KUFANYA MAPENZI KABLA YA NDOA /SEX BEFORE MARRIAGE..!

"SIWEZI KUUZIWA MBUZI KWENYE GUNIA.... "

BINTI HII ITAKUSAIDIA.......!

Kwa wanaume wenzangu pia mnaweza kusoma, na Mungu akipenda hivi karibuni ntaandaa ujumbe kwa ajili yetu.

(Forwarded and edited)
Mapenzi ya sasa yamekuwa kitendawili kisichoweza kujibika, yamewaacha wengi kwenye kilio na masikitiko yasiyoweza kubebeka.. Kwa kweli yana katisha tamaa, na katika hili mabinti ni waathirika wakubwa sana, mabinti wengi wana vidonda mioyoni mwao vibichi visivyo tibika kwa haraka.. Lakini kwa kuwa nawapenda na nimeamua kuwasaidia huu ni ujumbe wa MATUMAINI KWENU.

Dada yangu ni kweli umeumizwa, ni kweli una kilio kikubwa moyoni mwako hata kama si wewe basi rafiki yako au ndugu yako amepitia hali hii.. Lakin unajua nini chanzo cha kilio chako? Ulishawahi kujiuliza?

Unaweza ukasema ni kwa sababu kijana fulani alikuacha licha ya mapenzi na upendo mkubwa uliomuonesha..Sawa, nakubaliana na wewe kwa sehemu fulani, lakini labda nikusaidie. Maumivu uliyo nayo si kwa sababu fulani amekuacha bali ni kwa sababu umepoteza THAMANI yako kwa mtu asiye na maana.
Kivipi? Pindi uliporuhusu kukufunua sketi yako na kulala nae hapo ndipo ulipopoteza thamani yako kwake.

Mbaya zaidi baada ya kulala nae alipunguza upendo kwako, na kuanza kuwa na wanawake wengine na pengine kukuacha kabisa..Dada thamani yako na utu wako uliutoa hapo. Hata kama utavaa nguo za kujisitiri mwili ufunike mpaka macho mbele yake ni kama upo MTUPU usiyevaa kitu. Ni kipi asichokijua kwako? Kuanzia nywele zako mpaka kucha ya kidole chako cha mguu anakujua.. HUNA JIPYA KWAKE..!

Kosa lako ni kuruhusu kulala na wewe, hapo ndipo msiba wako ulipo, kama asingelala na wewe maumivu yasingekuwa kama yalivyo sasa. Unaweza ukaniuliza, 'Ningewezaje kujizuia kufanya nae Mapenzi?' Kwanza wanaume wanasema 'Hamuwezi kununua mbuzi kwenye gunia'
Dada yangu ni kweli huwa wanasema hivyo lakini JE WEWE NI MBUZI? Thamani yako ni sawa na mbuzi wa kuliwa liwa kirahis hivyo? Kama wewe ni mbuzi sawa basi endelea kuliwa. Haujui thamani yako na hayo ndiyo matokeo yake.

Nikusaidie hapo, mwanaume ni kama muwindaji na ili apate windo lake ambaye ni wewe lazima ajipange, sasa hiyo misemo ni mbinu tu za kukuingiza kwenye mtego. Kama umekubali kuingia kwenye mtego wa muwindaji na kuwa kitoweo chake, sawa.. NI UAMUZI WAKO ila jiandae kuwaalika watu kwenye msiba utakaoupata.

Labda nikusaidie tena hapa, mwanaume anapokuja kukutongoza kwa mara ya kwa upendo wake huwa ni asilimia mia moja (100%) wakati wewe upo na asilimia zero (0%), anapoanza kukupigia simu, kukutext, kukuomba out, na kuonesha care mbalimbali upendo kwako taratibu unaongezeka mpaka kufikia 40-50% ambapo utamkubalia na kuanza mahusiano rasmi, taratibu upendo utaendelea kuongezeka kwako na inapofikia umeSEX nae upendo wako unaweza ukajikuta umefika hadi 80-90% hapa sasa wewe ndio hujiwezi kwake, lakini kwa bahati mbaya kwa mwanaume upendo hushuka ghafla toka 100% mpaka 0-10%,20-30% na kwa wachache 40-50%.(inategemea na
mwanaume mwenyewe).

Naomba nielezee hapo kwenye hizo asilimia kwa wanaume. Kama ifuatavyo :
0-10% : Kundi hili ni la wanaume ambao ni wawindaji wazoefu (professional hunters), hawa hawana huruma wakisha'sex na wewe upendo hamna tena na wanakuacha ukiwa unalia na kujuta. Hawa kaa nao mbali.

20-30% :Hawa ni wale ambao baada ya sex upendo hupungua lakini wana utu kidogo, hawatakuacha ila watakuletea pozi na maringo, wata'date na watu wengine ila hawakutamkii kukuacha sasa Kazi kwako kubaki au kuondoka.

40-50% : Kundi hili, huwa wana utu na wastaarabu, upendo hupungua lakini bado wataku'care na kukuonesha heshima hata kama watakuwa na wasichana wengine basi ni kwa siri sana.. Wanaume wa Kundi hili hawatakutamkia kukuoa ila ukiwa na juhudi, upendo wa kweli unaweza ukawashawishi kufikiria ndoa.

Nadhan umepata picha kwa sehemu fulani, si lazima wanaume wote wawe kwenye makundi hayo 3, lakini wengi wao watakuwa hapo.

Ninachotaka kusema ni hiki. Ni UAMUZI ni wako dada, kuwa mbuzi kuliwa au kuweka msimamo na kujiamini. Unaweza ukasema lakini wanaume ni ving'ang'anizi, wanaume hawakubali kukuoa bila kuwa mimba, kama nikimnyima si ataniacha na kwenda kwa wanawake wengine?
Okay, may be you are right.. Lakini kama ukiweka msimamo wako akaamua kukuacha UJUE HUYO SI MWANAUME WA KUOA NI HUNTER (muwindaji), muache AENDE. BAKI NA MSIMAMO WAKO ACHA AKAWINDE KATIKA PORI LINGINE.


Dada yangu ni lini uliipoteza BIKRA yako? Tangu ulipoanza kufanya mapenzi ukiwa na miaka 14-16 mpaka leo umeshalala na wanaume wangapi? Hadi utakapoolewa utakuwa na orodha ya wanaume wangapi? IFIKE HATUA USEME "SASA BASI", JITHAMINI, JIHESHIMU, JIKUBALI NA JIAMINI. Kumbuka kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza na chanda chema huvikwa PETE. Ni kweli wanaume wengi watakukumbia na marafiki zako watakuona mshamba lakini HUTAKOSA MWANAUME WA KUKUOA.

ILA MSIMAMO WAKO PEKEE BILA MSAADA WA MUNGU UNAWEZA UKASHINDWA. MKABIDHI YESU MAISHA YAKO NAE ATAKUSHINDIA NA KUKUEPUSHA NA WAWINDAJI.

DADA YANGU, DUNIA IMEHARIBIKA, IMEZUNGUKWA NA WAWINDAJI HATARI WENYE KILA MBINU. UTAWEZAJE KUPONA?? YESU NDIYE MSAADA WAKO PEKEE.. MKUBALI SASA..!!

WEWE SIO MBUZI BALI NI MWANAMKE WA THAMANI MBELE ZA MUNGU....!

"MWANAMKE UNAWEZA UKIJITAMBUA... "
 
Umeandika mambo mazuri sana mpendwa.....lakini bahati mbaya ujumbe wako umeuleta wakati wahusika wameshafanya maamuzi ya kufanya vile mioyo yao inavyowatuma......

Tunaishi katika nyakati ambazo mwanadamu amepoteza umiliki wa akili yake.....na matendo yake yanaongozwa na matamanio ya moyo wake.....ni nyakati hatari sana....kwani kwenye kutimiza mahitaji ya moyo huku akili ikiwekwa pembeni lolote linaweza kufanyika.....na mengine yakiwa ni ya hatari zaidi....

Ni Mungu pekee ndio wa kutuokoa na kadhia hii....
 
Back
Top Bottom