Huu ni ugonjwa gani? Tiba yake je? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni ugonjwa gani? Tiba yake je?

Discussion in 'JF Doctor' started by KAUMZA, Feb 9, 2011.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Katika pita pita zangu nimekutana na kijana wa takribani miaka 20. Na katika kujenga nae mazoea akaniambia kuwa, amekuwa akiumwa kichwa kila mwezi unapoandama. Na kabla ya kichwa kuanza kuuma hutanguliwa na kupiga chafya mfululizo.

  Katika historia, mama yake ana matatizo ya ugonjwa wa kifafa. Aliponisimulia nilidhani labda na yeye amerithi tatizo la mamaye. Lakini nilipompeleka ktk hospitali ya mkoa aliambiwa kuwa hana ugonjwa huo.

  Unaweza kuwa ni ugonjwa gani na tiba yale ni nini hasa!!
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  ikiwa kama ni kweli kila mwezi unapoandama ndio huyo rafiki yako anaumwa na kichwa muulize kitu kimoja kwanza je yeye huyo rafiki yako ni Dini gani?

  akisema kuwa ni Muislam aende kwa Sheikh au imam wa Msikiti huyo imam amwambie amuombee duwa kwa kumsomea Suratil Fatihat (Alhamdu yote ) mara 40

  huku huyo imam amemshika kichwa rafiki yako akimaliza kumsomea amwache atulie kama dakika 10 kidogo kwa uwezo Wa Mwenyeezi Mungu atapona. La kama huyo rafiki yako ana

  Dini ya Kikristo mwambie aende kwa Mchungaji wa kanisa lake anapofanyia ibada akaombewe duwa na huyo Mchungaji atapona kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu huo ndio ushauri wangu
   
 3. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Shukran, hundred times
   
 4. k

  kamili JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60  Hicho ni kifafa, kwa bahati siku hizi uzoefu unaonesha kinatibika vizuri zaidi hospitalini kuliko tiba zingine. Mpeleke hosp. na uonane na daktari wa afya ya akili atapatiwa dawa ambazo atazitumia kwa muda mrefu kidogo hata kama hiyo shida itaacha mara tu.Atapona. kumbuka akichelewa dawa aweza athirika akili.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mkuu una uhakika hayo Maradhi yake ni kifafa? Mgonjwa amekwenda hospitalini Kuchunguzwa hakuonekana na hicho kifafa Mgonjwa sasa wewe unasema ni kifafa unaoushahidi wowote kuthibitisha kama ni kifafa?

  Dawa ingine Mkuu Kaumza Dawa ingine ya Maradhi ya kichwa ajaribu kutumia hii hapa > Maumivu ya kichwa Mwambie mgonjwa apakae Mafuta ya Kitunguu Saumu mahala panapouma kichwani,yatoondoka hayo Maumivu ya kichwa upesi. Halafu atakimeza kwa maji kitunguu Saumu punje moja ili aondowe chanzo cha Maumivu iwapo yapo ndani ya Mfuko wa kusaga chakula wa tumbo (Maida).

  Na ingine hii hapa Dawa ya Maumivu ya Kichwa Atachemsha Kitunguu Maji Kilichochambuliwa pamoja na karafuu iliyosagwa na iliokandwa katika Mafuta ya zeituni,ataiacha mpaka ipoe kisha ataisafisha na atachukuwa mafuta ya zeti asugue mahala panapouma na atakunywa kiasi cha kijiko kabla ya kulala. Tiba hii huipa nguvu mishipa.
   
Loading...