canular
JF-Expert Member
- Jan 7, 2018
- 1,068
- 1,268
Nina pinga kwa nguvu uhalali wa serikali , bunge , na uongozi wote kwa sababu ya wazi ya kukosekana kwa upigwaji kura halali. Serikali hii haijachaguliwa kwa njia za kidemokrasia, na hivyo kinyume na misingi ya uhuru na haki za kiraia za Watanzania.
Tunatambua haki yetu kama wananchi kuchagua viongozi wetu kupitia uchaguzi huru na wa haki , na kwa kukosekana kwa msimamo huu wa msingi, ninakataa kuitambua serikali yote, bunge, au uongozi usiofuata taratibu za kidemokrasia.
Ninatoa wito kwa jamii ya kimataifa, vyombo vya haki za binadamu, na wananchi wa Tanzania kwa umoja kusimama na kuunga mkono harakati za kutaka uhalali wa uongozi kupitia uchaguzi huru na wa haki.
Ninaomba mfate taratibu na mustakabali wa nchi yetu unaotegemea misingi ya demokrasia , haki , na uhuru wa wananchi . Sitakubaliana na mfumo wowote usiozingatia haki za msingi za Watanzania
Huu ni msimamo wangu kama mwananchi wa Tanzania ninaejitambua na kuamini katika demokrasia ya kweli na uwazi wa utawala. Asanteni