Sodoku
JF-Expert Member
- Feb 3, 2016
- 1,260
- 2,863
Pengine rekodi zifuatazo zinaweza zikawapa hasira zaidi mashabiki wa ‘Mnyama’ na hata kuwataka Viongozi wao kuhakikisha kuwa wanafanya kila linalowezekana ili timu yao hiyo iwe bingwa wa VPL 2015/2016.
Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi
Mapema mwaka huu (2015) Simba SC ilifanikiwa kuutwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar na hata kujikuta ikiweka rekodi adhimu zaidi ya kulitwaa taji hilo mara nyingi zaidi kuliko timu yoyote kutoka bara na visiwani.
Simba imetwaa taji hilo mara tatu, lakini pamoja na kufanya hivyo bado haijaweza kukata kiu ya mashabiki wake kuhusu kuuota ubingwa wa VPL na hata kuwafanya mashabiki wao kujikuta wakiwasurutisha Viongozi wao kufanya usajili wenye tija na siyo usajili wa ‘bora liende’.
Ubingwa Kombe la Kagame
Licha ya Yanga kujivunia rekodi ya kutwaa taji la Kagame nje ya Dar es Salaam, Simba ndiyo vinara wa kulitwaa taji hilo nchini. Simba imewahi kulitwaa taji hilo la Kagame mara sita na kuwa timu ya Bara yenye historia ya kulitwaa zaidi kombe hilo kuliko timu nyingine yoyote.
Mbali na kuwa timu ya Bara iliyotwaa taji hilo mara nyingi, Simba ndiyo timu inayoongoza kwa kutwaa Kombe la Kagame kwenye historia ya michuano hiyo na kuzipiku timu zote za ukanda huo.
Rekodi ya kucheza fainali ya Kombe la shirikisho (CAF)
Wekundu wa Msimbazi ndiyo timu pekee ya Tanzania iliyofanikiwa kucheza fainali za Kombe la Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika yaani CAF. Ilikuwa mwaka 1993 wakati huo likijulikana kama Kombe la Caf.
Simba ilicheza fainali hiyo na Stella Abidjan ya Ivory Coast na kutoka sare katika mchezo wa awali kabla ya kukubali kipigo cha mabao 2- 0 katika marudiano jijini Dar es Salaam.
Licha ya Simba kupoteza mchezo huo ambapo wachezaji wake waliahidiwa zawadi za magari kama wangeshinda, inasalia kuwa timu pekee kutoka Tanzania Bara iliyofanikiwa kucheza hatua hiyo ya fainali hizo.
Nusu fainali klabu Bingwa Afrika
Historia ya klabu ya Simba inavutia! Ndivyo unavyoweza kusema kwa lugha rahisi baada ya timu hiyo kufanikiwa kucheza nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 1974.
Hata hivyo iliondolewa katika hatua hiyo ya nusu fainali na klabu ya Mehala El Kubra ya Misri na kuzima ndoto za kucheza fainali ya michuano hiyo mikubwa zaidi katika bara la Afrika.
Rekodi hiyo ya Simba bado haijavunjwa mpaka leo hii ni timu yoyote ya Tanzania, japo mwenendo wake kwa sasa unaonekana kuwaghafilisha wanazi wengi wa timu hiyo kwa sasa.
Historia ya kuiondosha Mashindanoni timu ya Misri
Mbali na rekodi tajwa hapo juu ambazo huenda zikazidi kuchagiza machungu kwa mashabiki wa timu hiyo. Simba SC bado inajivunia rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kufanikiwa kuiondosha timu ya Misri katika michuano ya Afrika.
Wanaume hawa walifanya hivyo mwaka 2003 baada ya kuifunga Zamalek ya Misri ambayo ilikuwa inatetea ubingwa huo.
Pengine ninaweza nikawa nimewauzi mashabiki na wafuasi wengi wa klabu ya Simba kwa maelezo hayo machache kuhusu klabu ya Simba. Lakini siku zote ukweli huwa haujifichi.
Ni kweli rekodi na takwimu hizi tamu zinaifanya Simba ibaki kuwa na historia nzuri na ya kuvutia kimataifa lakini kwa sasa haina jipya kutokana na mwenendo wake usiotia matumaini.
Nitoe wito kwa viongozi husika kuhakikisha kuwa wanafanya usajili wenye tija zaidi kwa lengo la kukiboresha kikosi chao na hata kuweza kuirudisha heshima ya timu hiyo, heshima ambayo kwa sasa imeonekana kupungua.
Kwa nijuavyo mimi, hakuna linaloshindikana chini ya Jua. “Ni kweli imebaki historia! Ngoja tuusubiri msimu mpya wa Ligi huenda ikaja kivingine.
From O. Ngonyani