Eti Rais anatembea kwa kufanya mazoezi na inakuwa habari ya kutolewa magazetini na runingani! Yaani tunashangaa Rais kutembea, utadhani yeye ni malaika ambaye kwonekana ardhini ni maajabu! Eti kutembea! Kutembea?
- Ni Watanzania wangapi hutembea kila siku umbali mrefu kwenda kutafuta maji?
- Ni Watanzania wangapi hutembea umbali mrefu wakiwa wamebeba mizigo mizito vichwani wakienda sokoni, magulioni na mashambani?
- Ni vijana wangapi wahitimu wa vyuo watembeao kila siku kutwa wakiingia ofisi hii na ile kutafuta kazi?
- Ni Watanzania wangapi watembeao...........? (Ongeza mengine mwenyewe sasa)