Huu ndio uwanja wa fainali Azam Sports Federation Cup mjini Dodoma

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Baada ya uwanja utakaopigwa mchezo wa Fainali ya FA kujulikana, wadau wa soka wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya mahala itakapofanyika kwa fainali hizo ambazo zinawakutanisha klabu ya Soka ya Mbao Fc dhidi ya Wakongwe wa ligi Simba Sc, katika fainali hizo za 2017 (Azam Sports Federation Cup),

FA.jpg

Kabla ya uwanja wa Jamhuri-Dodoma kutajwa kuwa ndio utatumika kwa ajili ya fainali ya FA Cup, kulikua na mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii ambapo wadau wa soka nchini walikuwa wakijadili tweet ya Rais wa TFF kwamba kutakuwa na droo ya kutafuta uwanja utakaotukika kwa ajili ya fainali hiyo.

======

Hatimaye Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limeweka wazi uwanja utakaotumika kwa ajili ya fainali ya mchezo wa Fainali za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup HD - ASFC) mwaka huu.Hayo yamesemwa leo na Rais wa TFF Jamal Malinzi wakati akifungua kozi ya uamuzi na ukocha inayoendeshwa na Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ubungo (UFA) na kuweka wazi kuwa fainali ya Kombe la FA itafanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.

Fainali hiyo kati ya Simba SC ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza, itafanyika Mei 28, mwaka huu huku kila timu ikiwa ni wageni kwenye uwanja huo ambapo makao makuu ya nchi yanapatikana.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 5 ya michuano ya ASFC kuhusu Uwanja wa mashindano inasema: “Uwanja wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD utakuwa ni uwanja wenye hadhi inayokubalika na TFF.”

Hilo limekuja baada ya jana Rais wa TFF kunukuliwa katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter akisema kuwa, kutachezwa kwa droo ya kutafuta wapi fainali ya Shirikisho itachezwa huku wadau mbalimbali wakionekana kupinga suala hilo na kusema haiwezekani na haijawahi kutokea.

Simba walifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam mchezo ukiofanyika April 29 katika dimba la uwanja wa Taifa, na Mbao kuivua ubingwa Yanga kwa kuifunga goli 1-0 mechi iliyopigwa April 30 dimba la CCM Kirumba Mwanza.
 
Dodoma ...utaendelea kuwa mji wa maigizo tu, si wasubirie tu huo wa Mfalme wa Morocco uishe kwanza!?
 
Fainali itachezwa tu! Kama mlikuwa mnataka mkachezee Dar, mmebuma.

Kama nyie wanaume gomeni kwenda Jamhuri.
 
Dodoma ...utaendelea kuwa mji wa maigizo tu, si wasubirie tu huo wa Mfalme wa Morocco uishe kwanza!?
Mkuu na wewe unadhani kuna uwanja unajengwa na Mfalme wa Morroco kweli?

Ikiwa huko kwao juzi walikuwa wanalalamikia Deficit ya Viwanja? Hii ni ndoto kwa kweli.
 
Hizo mbao zinatengenezwa meza.Kama mnavyoomba nyie vyura.Ngoma itapigwa juu ya ubao na mbao zitavunjwa na uzito wa simba. Huo uwanja simba ameshautumia kabla ya hayo munayoomba.Ovyo kabisa nyie.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom