Huu ndio utaratibu wa kumpata Mbunge au Diwani viti Maalum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ndio utaratibu wa kumpata Mbunge au Diwani viti Maalum

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwakaboko King, May 6, 2017.

 1. Mwakaboko King

  Mwakaboko King JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2017
  Joined: Apr 22, 2015
  Messages: 1,081
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeeleza kuwa nafasi za Wabunge wa Viti Maalum wanaoteuliwa zipo kwa mujibu wa Sheria na zimeainishwa katika Ibara ya 78 (1) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

  Akitoa ufafanuzi huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amesema kuwa Ibara ya 78 (1) na (4) ya Katiba inaeleza utaratibu mzima wa kuwapata Wabunge wanawake wa Viti maalum.

  Amesema kila Chama cha Siasa kinachoshiriki katika Uchaguzi Mkuu na kupata angalau asilimia 5 ya Kura zote halali za wabunge kitapata Wabunge wa Viti Maalum kulingana na Kura kilizopata

  Amefafanua kuwa Chama kinachopata asilimia 5 ya Kura zote halali za Wabunge katika Uchaguzi Mkuu kinatakiwa kuwasilisha orodha ya wanachama wanaopendekezwa kuwa wagombea wa Viti Maalum ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

  Aidha, ameeleza kuwa endapo inatokea nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na sababu mbalimbali, Spika wa Bunge humtaarifu Mwenyekiti wa Tume juu ya uwepo wa nafasi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343

  Amesema kuwa Mwenyekiti wa Tume hukiandikia barua chama husika kukitaarifu juu ya uwepo wa nafasi wazi ya viti maalum ili kiweze kuwasilisha pendekezo la jina katika orodha kiliyowasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka 2015, ikiambatanishwa na Fomu namba 8 D ya kuomba jina lililopendekezwa liteuliwe na Tume katika nafasi ya Ubunge kulingana na vigezo vilivyoainishwa.
   
 2. BILGERT

  BILGERT JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2017
  Joined: Feb 27, 2015
  Messages: 1,910
  Likes Received: 1,518
  Trophy Points: 280
  Ufafanuz murua saana,
   
 3. Caroline Hans

  Caroline Hans JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2017
  Joined: Feb 7, 2017
  Messages: 629
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 80
  Vigezo na masharti lazima vizingatiwe
   
 4. Kinjekitile junior

  Kinjekitile junior JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2017
  Joined: Apr 20, 2015
  Messages: 4,319
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mkurugenzi uko vizuri !
   
 5. mguu ndama

  mguu ndama JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2017
  Joined: Mar 29, 2017
  Messages: 264
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 60
  Na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi anapatokanaje?
   
 6. Mwakaboko King

  Mwakaboko King JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2017
  Joined: Apr 22, 2015
  Messages: 1,081
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ibara ya 74.-(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 imeweka utaratibu wa kumpata Mwenyekiti wa Tume
   
Loading...