Huu ndio ulinzi shirikishi?

Huu ndio ulinzi shirikishi?

jakamot

Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
51
Reaction score
4
Maeneo ya mtaa wa kibini musoma mjini ulinzi shirikishi wanakamata watu na kuwanyang'anya vitu mbalimbali, kuna jamaa alikamatwa mnamo saa tano za usiku, akaombwa kutoa pesa alipokataa waliamua kumsachi na kuchukua pesa zote alizokuwa nazo ndipo wakamwachia.Hii ni sawa?
 
Hao ni waharifu tu, wanataka kuharibu dhana ya ulinzi shirikishi ambayo maudhui yake ni mazuri sana ambapo mpaka sasa uhalifu umeshuka kasi tangu kuanzishwa kwa polisi jamii. kama mnawajua hao watu toeni taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa husika ili wakamatwe huo ni uhalifu kama ulivvyo uhalifu mwingine,
 
Wizi shirikishi huo! Wengine wanajifanya matrafic siku hizi, wanaomba waonyeshwe lesseni.
 
Ndo wezi wa usiku waliohalalishwa na Jamii,,,mi kuja jamaa yangu alikutana nao mtaani alizunguka nao mpaka Alfajir kisa hakutoa hela...
 
Usiku ndio huwa wanapita ila siku hizi hata sijawasikia

wananipaga risiti,ni huku UDSM Maeneo ya Changanyikeni sijui ka unakupata
Good Mwenzetu, kweli sikupati lakini I hope uaminifu upo na usalama unashamiri kwenu...
Good luck
 
Maeneo ya mtaa wa kibini musoma mjini ulinzi shirikishi wanakamata watu na kuwanyang'anya vitu mbalimbali, kuna jamaa alikamatwa mnamo saa tano za usiku, akaombwa kutoa pesa alipokataa waliamua kumsachi na kuchukua pesa zote alizokuwa nazo ndipo wakamwachia.Hii ni sawa?

Hapana. Huu si ulinzi shirikishi. Jina lake la kitaalamu unaitwa "WIZI SHIRIKISHI".
 
Maeneo ya mtaa wa kibini musoma mjini ulinzi shirikishi wanakamata watu na kuwanyang'anya vitu mbalimbali, kuna jamaa alikamatwa mnamo saa tano za usiku, akaombwa kutoa pesa alipokataa waliamua kumsachi na kuchukua pesa zote alizokuwa nazo ndipo wakamwachia.Hii ni sawa?

Hapo Kibini hakuna walinzi shirikishi wote hao ni wezi tu! Mimi naishi mitaa hiyo hiyo jirani na kwa Mamaz hapo Nyasho shuleni! Manake vijana wengi waliojitokeza na kuchaguliwa kufanya hiyo kazi ni wale waliokuwa wapambe wa mbunge wa zamani wa Musoma mjini Mathayo kabla hajapigwa chini na wananchi japo alimwaga pesa nyingi ili achaguliwe, hatimaye mheshimiwa Vicent Nyerere akapewa ridhaa ya kuwawakilisha wananchi!

Wapambe hao wahuni waliunda kundi lililojulikana kama Jamaica Mockers, ambalo lilikuwa linavamia watu majumbani usiku, kujeruhi, kuiba na kubaka! Masalia ya baadhi yao ndiyo wanaojifanya walinzi shirikishi hapo Kibini ambapo hapaishi matukio ya ujambazi mara kwa mara!!
 
Back
Top Bottom