Huu nao ni UDHAIFU...

hansmak

Member
Feb 24, 2015
25
28
Kama wanafunzi wanapiga kelele darasani na kiongozi wa darasa (ambae ndie muangalizi na mdhibiti namba moja wa nidhamu na mienendo ya wanafunzi wenzake darasani) ameandika majina ya waliopiga kelele darasani (katimiza wajibu wake kama kiongozi wa darasa)kisha akapeleka kwa mwalimu wa darasa ili achukue hatua dhidi ya wale wote waliopiga kelele darasani.Kama mwalimu kashindwa kuchukua hatua (japo kwa kujaribu) basi huo utakua UDHAIFU wa mwalimu wa darasa kushindwa kulisimamia darasa lake vizuri na zaidi ya yote kushindwa kuchukua hatua dhidi ya wapiga kelele darasani (japo kaletewa majina ya wapiga kelele darasani). Tabia hii ikiachwa iendelee basi itaenea darasa zima na kama hatua stahiki zikishindwa kuchukuliwa na mwalimu husika(mwalimu wa darasa) basi inaeweza kuenea shule nzima na hatimae kila mwanafunzi atafanya lile analohisi ni sahihi kwa wakati huo bila kuangalia sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya shule husika inasemaje.
Hali ikishakua hivi, basi jua kwamba anaestahili kuchukua hatua na kufanya maamuzi mazito ili kurudisha nidhamu ya wanafunzi ni mkuu wa shule na jopo lake. Lakini kama mkuu wa shule nae atashindwa kuchukua hatua (japo kaambiwa, anaona na ameletewa ushahidi na baadhi ya wanafunzi wanaohusika) basi huo utukua ni UDHAIFU wa mkuu wa shule na jopo lake.
 
Mwalimu mkuu anahusika na kelele za wanafunzi maana darasa husika lipo mkabala na ofisi ya mwalimu mkuu.
 
Tatizo mwalimu mkuu hawapatani na yule kiranja wa darasa sasa mwalimu wa darasa inamlazimu kutoonesha ushirikiano na kiranja wake wa darasa ili kumlidhisha mwalimu mkuu.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom